title : MIAKA 70 YA NAKBA YA WANANCHI WA PALESTINA
kiungo : MIAKA 70 YA NAKBA YA WANANCHI WA PALESTINA
MIAKA 70 YA NAKBA YA WANANCHI WA PALESTINA
Taifa letu la Palestina linaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 ya Nakba (janga), likiendeleza mapambano kabambe ya kurudisha haki zake thabiti za kizalendo, kuondoa athari na matokeo yake ambayo bado yapo katika nyanja zote za maisha ya taifa letu. Hiyo ni tangu utekaji wa ardhi yote ya Palestina ya kihistoria hadi kuwatoa nusu ya wananchi wa Palestina nje ya nchi yao.
Kwa yakini mapambano ya kitaifa kwa ajili ya ukombozi yatathibitisha malengo yake hata kama ni kwa muda mrefu, licha ya uadui wa utekaji na uhalifu wake unaoendelea, na licha ya uungaji mkono wa Marekani uliopitiliza chini ya Rais wake Donald Trump kwa taifa tekaji la Israel, hasa uamuzi wake wa kusikitisha wa kuizingatia Jeruselemu kuwa ni mji mkuu wa taifa tekaji na kuhamishia ubalozi wa Marekani mjini Jerusalemu, jambo linalokiuka sheria ya kimataifa na maazimio yake, pia ni jambo linaloifanya Marekani kuunga mkono utekaji na uadui dhidi ya wananchi wa Palestina na suala lake la kizalendo.
Kama ilivyo kila mwaka tarehe 15 Mei, wananchi wetu popote pale walipo kwa nguvu za kizalendo na taasisi zake huikumbuka kumbukumbu hii yenye kuumiza kwa shughuli na harakati mbali mbali. Lakini mwaka huu unashuhudia mabadiliko makubwa na muhimu katika kuutukuza mnasaba huu, kwani inaenda sambamba na safari kubwa ya kurejea iliyoanza tangu wiki kadha kwenye mipaka ya kihistoria ya Palestina pamoja na ukanda wa Gaza.
Makumi ya watu wamekufa mashahidi na maelfu wamejeruhiwa. Kilele chake kitakuwa tarehe 14 -15 Mei, hii kwa kuthibitisha wananchi wetu wameshikamana na malengo na haki zake za kizalendo na mbele kabisa haki yake ya kurudi vijijini kwao na mali zao; na haki ya kusimamisha taifa lake huru lenye heshima kamili katika mji wake mkuu Jeruselemu, pamoja na kuondolewa kuzingira kuovu katika ukanda wa Gaza.
Ukweli msimamo wa Marekani na hatua iliyoichukua mnamo Januari mwaka huu, wa kupunguza msaada wake kwa UNRWA kwa kiasi cha dola za kimarekani millioni 65 toka kile kiasi inachokitoa kwa UNRWA. Uamuzi huu kwa taifa letu umepelekea hofu kwa suala la wakimbizi kwa kujaribu kulifuta na kuliweka hatarini kwa masilahi ya msimamo mkali wa serikali ya Israel ambao unajitahidi kwa nguvu zote kulitokomeza suala la wakimbizi ambalo ndio kiini cha suala la Palestina. Hiyo ni kukausha vyanzo vya misaada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia na kuwahudumia wakimbizi wa Palestina (UNRWA), hadi kufikia kuliondoa kikamilifu.
Katika kumbukmbu ya 70 ya Nakba (janga) ya Palestina,majukumu yetu wote yanaongezeka kuhusiana na suala letu la haki,katika ulazima wakupambana na kukabiliana na maelezo ya kizayuni na kiizraeli kuhusu Nakba lililowakumba Wananchi wa Palestina, ambalo limepelekea kuhamishwa maelfu ya wapalestina, hasa kile kilichojumuishwa na “Mpango wa Dalet” uliopitishwa na Shirika la Kizayuni mwanzoni mwa mwaka 1948 na kuachiwa utekelezaji wake Haganah (kikundi cha mauaji na utesaji) kwa muongozo wa uwazi,kama vile kuua,kuhofisha,kuzingira miji na vijiji vya palestina,kuchoma nyumba na mali,kuzika mabomu katika vifusi ili kuwazuia wenyeji kurejea Kartika nyumba zao.
Vikundi vya hagana na jumuiya zingine za kizayuni kufuatia mpango huo zimetekeleza mauaji 28,huku mauaji mabaya zaidi katika hayo ni yale ya mjini Deir Yassin mnamo tarehe 9 April 1948. Hii ni pamoja na kuvunjwa na kuteketezwa miji na vijiji 531,kuhamishwa wapalestina laki nane (8) waliofanywa kuwa ni wakimbizi katika nchi yao, ni sawa waliokuwa katika ardhi ya mwaka 48,Ukingo wa Magharibi au Ukanda wa Gaza.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MIAKA 70 YA NAKBA YA WANANCHI WA PALESTINA
yaani makala yote MIAKA 70 YA NAKBA YA WANANCHI WA PALESTINA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MIAKA 70 YA NAKBA YA WANANCHI WA PALESTINA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/miaka-70-ya-nakba-ya-wananchi-wa.html
0 Response to "MIAKA 70 YA NAKBA YA WANANCHI WA PALESTINA"
Post a Comment