title : Maandalizi ya ukarabati wa Beit El Ajaib yaiva
kiungo : Maandalizi ya ukarabati wa Beit El Ajaib yaiva
Maandalizi ya ukarabati wa Beit El Ajaib yaiva
Na Salum Vuai, WHUMK
MAANDALIZI ya matengenezo ya jengo la Beit Al Ajaib lililoko Forodhani mjini Zanzibar yameanza kufuatia ziara ya ujumbe kutoka Wizara ya Urithi na Utamaduni ya serikali ya Oman.
Ujumbe huo unaoongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Salum Mohammed Mahruki, uliwasili nchini jana Mei 11, na leo ulitembelea jengo hilo kujionea hali halisi ya uchakavu uliosababisha lisite kutumika kama kivutio cha utalii kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
Msafara wa timu hiyo pia umemjumuisha mshauri mwelekezi ambaye ni mtaalamu wa uhifadhi majengo Dk. Enrico d’Errico, ambaye amekuja mahsusi kushauri njia bora ya kulitengeneza jengo hilo na mengine ya kihistoria nchini.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyowashirikisha watendaji wakuu wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Katibu Mkuu wa Wizara ya Urithi na Utamaduni ya Oman Salum Mohammed Mahruki, aliomba jengo hilo lisafishwe haraka, wakati wataalamu wakifanya tathmini ya kina ili kujua ukubwa wa kazi hiyo.
“Kwa namna tulivyoliona jengo hili, ni lazima kazi ya kulitengeneza ianze haraka iwezekanavyo, vyenginevyo tutazidi kuchelewa kwani tayari muda mwingi umepotea tangu lilipopata hitilafu,” alisisitiza.
Alifahamisha kuwa, sura ya Mji Mkongwe wa Zanzibar inaongezewa haiba na kuwepo kwa jengo hilo, ambalo kila mtalii anayefika anastaajabishwa na kuvutiwa na utaalamu pamoja na malighafi zilizotumika kulisimamisha tangu mwaka 1883.
OFISA Mkuu wa Idara ya Makumbusho Abdalla Magofu (aliyeshika mwamvuli), akitoa maelezo kwa ujumbe kutoka serikali ya Oman juu ya hali ya jengo la Ngome Kongwe lililoko Forodhani mjini Zanzibar. Kulia kwa ofisa huyo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Urithi na Utamaduni nchini Oman, Salum Mohammed Mahruki.
MSHAURI Elekezi na mtaalamu wa uhifadhi majengo kutoka Wizara ya Urithi na Utamaduni nchini Oman Dk. Enrico d’Errico (kushoto), akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Salum Mohammed Mahruki na wajumbe wengine, walipolitembelea jengo la Beit El Ajaib mjini Zanzibar, ambalo serikali ya Oman inakusudia kulifanyia matengenezo makubwa.
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe Zanzibar Issa Sariboko Makarani, Katibu Mkuu wa Urithi na Utamaduni wa Oman, watendaji wakuu wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, wakiliangalia kwa nje jengo la Makumbusho ya Kasri Forodhani mjini Unguja, walipofanya ziara kukagua majengo ya kihistoria yanayohitaji kufanyiwa matengenezo.
Hivyo makala Maandalizi ya ukarabati wa Beit El Ajaib yaiva
yaani makala yote Maandalizi ya ukarabati wa Beit El Ajaib yaiva Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Maandalizi ya ukarabati wa Beit El Ajaib yaiva mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/maandalizi-ya-ukarabati-wa-beit-el_15.html
0 Response to "Maandalizi ya ukarabati wa Beit El Ajaib yaiva"
Post a Comment