title : KIROBA CHA MAHINDI CHAGANDA KICHWANI KWA KIJANA ALIYEKIIBA MLANDIZI
kiungo : KIROBA CHA MAHINDI CHAGANDA KICHWANI KWA KIJANA ALIYEKIIBA MLANDIZI
KIROBA CHA MAHINDI CHAGANDA KICHWANI KWA KIJANA ALIYEKIIBA MLANDIZI
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
KIJANA Frank Joseph (25) ,mkazi wa Dar es salaam amezua gumzo huko Mlandizi mjini Kibaha mkoa wa Pwani baada ya kiroba cha mahindi cha kilo 20 alichoiba nje ya nyumba ya mama mmoja kumganda kichwani kwa zaidi ya saa nne leo Mei 3, 2019 majira ya saa 12 asubuhi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shanna alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa walizipata kutoka kwa mwenyekiti Ally Nyambwilo, na kwamba baada ya taarifa hizo walifika eneo la tukio na ambapo walifanikiwa kumuokoa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa hatarini kushambuliwa na wananchi.
Kamanda Shanna alieleza kuwa askari polisi walimchukua mtuhumiwa ambaye aliwaonyesha alikochukua mzigo huo lakini mwenye nyumba hakuwepo muda huo, hivyo mtuhumiwa alipelekwa kituoni akiwa na mzigo kichwani wakati harakati za kumpata mmiliki zikiendelea.
Aidha Kamanda Shanna alisema, mmiliki wa mzigo huo alipofika kituo cha polisi Mlandizi alionana na mtuhumiwa huyo na kumfungua zipu ya suruali na kuongea maeneo yake na baadae mtuhumiwa alipoambiwa ashushe mzigo ukitoka kichwani ukabanduka.
Kamanda Sganna aliwaonya vijana kuacha kuvuna vitu ambavyo hawakupanda na badala yake wajishughulishe kupata mali kwa jasho lao.
Frank Joseph alikiri kuiba mzigo huo ambao uligoma kushuka kichwani hadi mhusika alipofungua zipu ya suruali ndipo akapata wepesi kuushusha mzigo huo.
"Nilikua napita nikaona mzigo upo nje nikaubeba nilivyokua naushusha haukutoka kichwani na ulivyogoma kutoka nikaamua kurudi kwa mwenyewe lakini sikumkuta hadi nilipomuona kituo cha polisi alivyofungua zipu ya suruali yangu na kuongea maneno yake nikaweza kuushusha mzigo" alisema
Mtuhumiwa huyo alisema alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani!
Hivyo baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu na alipochoka alilazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi.
Frank ambae alidai anafanya kazi ya kusukuma mkokoteni ambapo aliwashauri vijana kuacha tamaa na kufanya kazi zao kwa bidii na kwamba hawezi kurudia tena kuiba baada ya tukio hilo.
Mtuhumiwa anaedaiwa kuiba kiroba cha mahindi chenye kilo 20 huko Mlandizi Kibaha Mkoani Pwani Frank Joseph akiwa kituo cha polisi cha Mlandizi mkoa wa Pwani alikofikishwa huku akiwa na mzigo uliomganda kichwani na ni hadi alipofika mwenye nao ndipo uliposhuka kichwani
Kamanda wa polisi mkoani Pwani ACP Jonathan Shanna (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha polisi Mlandizi kuhusiana na tukio la wizi ambapo kijana Frank Joseph (23) aliiba kiroba cha mahindi chenye kilo 20 huko Mlandizi Kibaha ambapo baada ya kuiba mzigo uliganda juu ya kichwa mwenye nao alipofika na kuushusha.
Picha na Mwamvua Mwinyi
Hivyo makala KIROBA CHA MAHINDI CHAGANDA KICHWANI KWA KIJANA ALIYEKIIBA MLANDIZI
yaani makala yote KIROBA CHA MAHINDI CHAGANDA KICHWANI KWA KIJANA ALIYEKIIBA MLANDIZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIROBA CHA MAHINDI CHAGANDA KICHWANI KWA KIJANA ALIYEKIIBA MLANDIZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/kiroba-cha-mahindi-chaganda-kichwani.html
0 Response to "KIROBA CHA MAHINDI CHAGANDA KICHWANI KWA KIJANA ALIYEKIIBA MLANDIZI"
Post a Comment