title : Kamati ya Bunge ya Uganda Yamwagia Sifa Mradi wa DMDP
kiungo : Kamati ya Bunge ya Uganda Yamwagia Sifa Mradi wa DMDP
Kamati ya Bunge ya Uganda Yamwagia Sifa Mradi wa DMDP
Kamati ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kutoka Nchini Uganda (PAC-LG) imemwagia sifa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam unaoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Tano za Mkoa wa Dar es salaam.
Kamati hiyo yenye zaidi ya wajumbe kumi waliotemebelea Mradi wa DMDP unaotekelezwa chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wamesema ni mradi wa mfano na kuigwa na Nchi za Afrika Masshariki zinazopata mkopo wa fedha kutoka Benki ya Dunia.
Akizungumza katika ziara hiyo ya mafunzo Mwenyekiti wa Kamati hiyo (PAC-LG) Mhe. Ronald Reagan Okumu amesema lengo la ziara yao ni kuona namna ambavyo miradi ya Uboreshaji Miundombinu inayotekelezwa kwa fedha za Mkopo toka Benki ya Dunia;
“Tunapenda kuona ubora wa miradi hiyo, taratibu za ulipaji fidia zilivyofuata, maelekezo ya mkopo wa fedha hizo yalivyozingatiwa na zaidi namna ambavyo fedha zilivyopokelewa, zinavyosimamiwa na wataalamu, zinavyotumika na zinafanyiwa ukaguzi na zaidi suala zima la thamani ya fedha”Value for Money” kuonekana katika miradi hiyo” alisema Mhe. Okumu.
Akipokea ujumbe huo toka Bunge la Uganda Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege amesema mradi huu umetekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu sasa na mafanikio yaliyopatikana ni makubwa na kwa kiasi kikubwa umesaidia kuwapunguzia kero wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam.
“Karibu mjifunze kwa kuona mtaona barabara zilivyojengwa kwa ubora wa hali ya juu, njia za bora waenda kwa miguu, mifereji yenye viwango ya kusafirishia maji ya mvua, masoko na ofisi za miradi pamoja na maabara za kisasa za kupima ubora wa barabara zinazoendelea kujengwa “ alisema Kandege.
Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege (kushoto) akiwapokea wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa toka Nchini Uganda waliotembela Wizara kuona ubora wa miradi ya Benki ya Dunia inavyotekelezwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda (PAC-LG) Mhe. Ronald Reagan Okumu (kulia) akiwa na mjumbe wa Kamati hiyo toka Uganda wakifuatilia kikao na Naibu Waziri wa Tamisemi(hayupo pichani) Mhe. Joasephat Kandege.
Wataalam wanaosimia Miradi ya Benki ya Dunia OR-TAMISEMI pamoja na Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda wakimskiliza mtaalamu wa maabara ya mradi wa DMDP.
Wataalam wanaosimia Miradi ya Benki ya Dunia OR-TAMISEMI pamoja na Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda wakimskiliza mtaalamu wa maabara ya mradi wa DMDP.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Kamati ya Bunge ya Uganda Yamwagia Sifa Mradi wa DMDP
yaani makala yote Kamati ya Bunge ya Uganda Yamwagia Sifa Mradi wa DMDP Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kamati ya Bunge ya Uganda Yamwagia Sifa Mradi wa DMDP mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/kamati-ya-bunge-ya-uganda-yamwagia-sifa.html
0 Response to "Kamati ya Bunge ya Uganda Yamwagia Sifa Mradi wa DMDP"
Post a Comment