title : HABARI KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI
kiungo : HABARI KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI
HABARI KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI
Na Khadija Khamis – Maelezo 14/05/2018
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe, Mohamed Aboud Mohamed amesema serikali inathamini asasi zisizo za kiserikali kama ZAPHA+ katika kusaidia mapambano dhidi ya ukimwi ili kuhakikisha maambukizi mapya yanapungua hasa kwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24.
Hayo ameyasema wakati akijibu suala la Mhe.Omar Seif Abeid wa Jimbo la Konde huko katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuzisaidia jumuiya kama ZAPHA+ ambazo zinajitolea kuhamasisha vijana kwenye mapambano na maambukizo ya virusi vya ukimwi ?
Amesema kuanzishwa kwa klabu maalum za Wilaya Micheweni na ZAPHA+ zenye lengo la kuwasaidia vijana wanaoishi na VVU ni jambo la kupongezwa na la kupigiwa mfano hii itasaidia kwa serikali na asasi zisizo za kiserikali kupata takwimu sahihi ya maambukizi mapya ya ukimwi.
Aidha alisema kupitia Tume ya Ukimwi na Wizara ya Afya inashirikiana pamoja na Jumuiya ya ZAPHA+ katika kuhakikisha kuwa inawajengea uwezo vijana ambao wanaoishi na virusi vya ukimwi kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali ,kuwapa fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi midogo midogo ,elimu juu ya ushauri nasaha matumizi sahihi ya kupunguza makali ya VVU pamoja na kuwapa misaada ya chakula pale fursa zinapojitokeza .
Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir amesema kasi ya engezeko la Idadi ya watu katika Wilaya ya Magharibi A na B Iinasababisha kukosekana kwa huduma za kijamii ikiwemo elimu, maji, miundombinu ya barabara na huduma nyenginezo .
Amesema ongezeko hilo la watu haliendi sambamba na ukuwaji wa uwekezaji katika miundombinu iliyopo na kushindwa kukidhi mahitaji halisi ya wananchi waliyopo katika wilaya hizo serikali baada ya kulitambua hilo ikaendelea na hatua za kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamiii kwa kuzingatia mipango na mipaka ya utawala iliyopo.
Aliyasema hayo wakati akimjibu Mhe. Machano Othman Said Jimbo la Mfenesini aliyetaka kujua jinsi ya ongezeko la watu wasiopungua 350,000 kwa mujibu wa sensa za 2012 idadi ambayo inaengezeka kila siku, Je Serikali haiyoni kwamba wakati umefika sasa wa kuanzisha mkoa wa kiserikali kama kilivyoamua Chama cha Mapinduzi?
Aidha alisema hakuna mikakati mahsusi ambao serikali imeiweka kwa ajili ya kuondoa kero za wananchi wa wilaya hizo badala yake serikali inaendelea kutatua kero za wilaya hizo kwa kuzingatia dira ya 2020 ya mpango mkuu wa kitaifa mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini MKUZA na ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi ya 2015 -2020 .
Alifahamisha kuwa katika utekelezaji wa mikakati hiyo ya kitaifa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaimarisha huduma za kijamii kwa wilaya zote za Unguja na Pemba katika sekta ya elimu ,Afya pamoja na miundombinu ya barabara.
MWISHO
IMETOLWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO.
Hivyo makala HABARI KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI
yaani makala yote HABARI KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HABARI KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/habari-kutoka-baraza-la-wawakilishi.html
0 Response to "HABARI KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI"
Post a Comment