DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI

DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI
kiungo : DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI

soma pia


DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI

Na Rhoda Ezekiel Kigoma ,

MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala ameagiza kukamatwa watu wote wanajihusisha na unywaji wa pombe za kienyeji nyakati za kazi huku akifafanua ulevi kupita kiasi ni moja ya mambo yanayochangia kukwamisha maendeleo.

Amesema inasikitisha kuona baadhi ya wananchi kunywa asubuhi badala ya kwenda kwenye shughuli za kimaendeleo.

Hali hiyo ilimlazimu Kanali Ndagala kuagiza Ofisa wa Polisi kuwakamata watu wote waliokuwa wanakunywa pombe katika vilabu vya pombe ya kienyeji nyakati za asubuhi. Pia ametoa maagizo ya Mgambo wawili kunyang'anywa vitambulisho vyao katika Kijiji cha Muhange baada ya kuwashuhudia wakinywa pombe asubuhu.

Ametoa maagizo hayo jana alipokwenda kijijini hapo kwa ajili ya kukagua na kuunga mkono shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya Sekondari katika eneo hilo.Amesema anasikitishwa kuona watu wana shindwa kufanya shughuli za maendeleo na kuanza kunywa pombe asubuhi na wengi wao wakiwa ni vijana.

"Wakati wenzao wakijitolea katika ujenzi wa shule ya Sekondari ili kutatua changamoto ya wanafunzi wa kata hiyo kutembea umbali mrefu ili kufuata shule ilipo ambapo wananchi wameanza juhudi zao na serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za wananchi,wao wanakwenda kwenye ulevi na hili hatuwezi kulivumilia," amesema.

Aidha Mkuu huyo amewataka wenyeviti wa vijiji vyote kuhakikisha vilabu vya pombe vyote vinafunguliwa kuanzia saa 10 jioni baada ya watu kumaliza kazi zao na wazingatie hilo na kuendelea kuwachukulia hatua za kinidhamu wale wote wanaokiuka sheria hiyo kwani ndio chanzo cha kuwa vibaka na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi na Serikali kwa ujumla.

" Ni aibu sana kuona vijana wadogo ambao mnanguvu za kufanya kazi kuja kunywa pombe asubuhi mnashindwa kufanya kazi.Ofisa wa Polisi hakikisha unawakamata hawa wote wanaokunywa na waliolewa muda wa kazi, sisi tunakuja kuhimiza maendeleo, wao wanaendelea katurudisha nyuma.


Baadhi ya Wananchi waliokamatwa kufuatia unywaji pome asubuhi badala ya kujishughulisha na shughuli za kimaendeleo.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akijionea mazingira halisi ya unywaji pombe asubuhi subuhi kwa baadhi ya wananchi kwenye moja ya vilabu vyao vya pombe
MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Wananchi huku akiagiza kukamatwa kwa watu wote wanaojihusisha na unywaji wa pombe za kienyeji nyakati za kazi huku akifafanua ulevi kupita kiasi ni moja ya mambo yanayochangia kukwamisha maendeleo.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akishiriki ujenzi na kuunga mkono shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya Sekondari katika eneo hilo.Amesema anasikitishwa kuona watu wana shindwa kufanya shughuli za maendeleo na kuanza kunywa pombe asubuhi na wengi wao wakiwa ni vijana.



Hivyo makala DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI

yaani makala yote DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/dc-kakonko-apiga-marufuku-unywaji-pombe.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI"

Post a Comment