title : WWF YAZINDUA MRADI WA KUHIFADHI MAZINGIRA-MTWARA
kiungo : WWF YAZINDUA MRADI WA KUHIFADHI MAZINGIRA-MTWARA
WWF YAZINDUA MRADI WA KUHIFADHI MAZINGIRA-MTWARA
Na Joseph Mpangala-Mtwara
Shirika la Kuhifadhi mazingira duniani WWF imezindua Mradi wa Kuleta mabadiliko katika usimamizi na Uendelezaji wa Maliasiri za misitu,wanyapori na bahari kwa kushirikisha Asasi za Kiraia pamoja na Wananchi katika mikoa ya Kusini.
Mradi huo wa miaka mitano unagharimu zaidi ya shilingi Billion10 fedha ambazo ni msaada kutoka shirika la maendeleo la SIDA kutoka Nchini Sweden kwa lengo la kusaidia Serikali na wananchii katika Kuboresha Usimamizi wa maliasili.
Akiongea katika Uzinduzi wa Mradi huo Mkurugenzi wa shirika la WWF hapa Nchini Dk.Amani Ngusaru amesema katika Mradi Utawezesha akina mama na Vijana ili kuhakikisha wanachochea mabadiliko katika katika usimamizi wa maliasili kwa ajili ya matumizi ya Vizazi vya sasa na Vijavyo.
Dr.Amani ameongeza kuwa Bado Maliasiri zetu zinakabiliwa na Changamoto ya Uharibifu unaochangiwa na Ongezeko la Shughuli za kibinadamu.
“katika hivi karibuni kumekuwepo na uvamizi mkubwa wa maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya shughuli za Kilimo,Malisho ya Mifugo,Uchimbaji wa madini,ukataji wa miti mjanga ya moto pamoja na uvunaji wa misitu ya asili kwa ajili ya ujenzi”amesema Dk.Amani.
Mradi huu unaafanyakazi katika mikoa ya Lindi,Rumuma pamoja na mtwara.
Mkurugenzi wa WWF hapa nchini Dr.Amani Ngusaru akiongea na wawakilishi wa asasi mbalimbambali za kiraia wakati wa uzinduzi wa Mradi wa uendelezaji Maliasili Mkoani Mtwara.
.Kaim Mkurugenzi wa Tunduru Jonathan A Haule wakatikati akionesha Kitabu cha WWF mara baada ya kufanya Uzinduzi wa Mradi wa Uendelezaji wa maliasi katika mikoa ya kuzini
Hivyo makala WWF YAZINDUA MRADI WA KUHIFADHI MAZINGIRA-MTWARA
yaani makala yote WWF YAZINDUA MRADI WA KUHIFADHI MAZINGIRA-MTWARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WWF YAZINDUA MRADI WA KUHIFADHI MAZINGIRA-MTWARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/wwf-yazindua-mradi-wa-kuhifadhi.html
0 Response to "WWF YAZINDUA MRADI WA KUHIFADHI MAZINGIRA-MTWARA"
Post a Comment