title : MAKALA SHERIA: POLISI HAWARUHUSIWI KUCHUKUA KESI ZA KUDAIANA HELA
kiungo : MAKALA SHERIA: POLISI HAWARUHUSIWI KUCHUKUA KESI ZA KUDAIANA HELA
MAKALA SHERIA: POLISI HAWARUHUSIWI KUCHUKUA KESI ZA KUDAIANA HELA
Yapo mambo tunatakiwa kuyazungumza mara kwa mara ili watu wayaelewe. Moja ya mambo hayo ni hili la watu kudaiana hela hadi kufikishana polisi. Mtu binafsi, Saccos au taasisi imekukopesha fedha, na hatimaye umeshindwa kulipa, wanachokifanya ni kukupeleka polisi. Huko polisi ati unaandikishwa maelezo na wakati mwingine unatakiwa kusaini mkataba mpya wa lini na namna gani utalipa deni.Au wakati mwingine unawekwa ndani kabisa, au huwekwi ndani ila siku ambayo umeambiwa kulipa ikifika hujalipa ati askari anakupigia simu kukuuliza kwa nini hujalipa deni , na vitisho vya kukukamata na kukuweka ndani, au wakati mwingine unakamatwa kabisa na kuwekwa ndani.
Kwa ufupi haya yote ni makosa makubwa. Ni makosa kwa askari yeyote ambaye ameamua kuchukua kesi ya aina hii, na ni makosa hata kwa yule anayedai ambaye amekwenda kuripoti .
1.KUDAIANA HELA.
Masuala ya kudaiana hela ni masuala ya madai(civil). Polisi hawahusiki kabisa na masuala ya madai. Polisi wanahusika na masuala ya jinai(criminal). Kudai hela si masuala ya jinai hata kidogo. Masuala ya jinai wanayohusika nayo polisi ni yale yote yaliyoorodheshwa katika Sheria ya Kanuni za adhabu, Sura ya 16 ambayo ni kama kubaka,kuiba, kutukana, kulawiti,kupigana, kuharibu mali , kujeruhi, rushwa, dawa za kulevya, uhaini, mauaji, kughushi, na mengine yaliyo katika sheria nyingine mtambuka yanayofanana na hayo.
2. HATA KUWEKWA CHINI YA ULINZI TU KWA MADAI YA HELA HAIRUHUSIWI.
Kutoruhusiwa kwa polisi kujihusisha na masuala haya ya madai ya kudaiana hela kumeelezwa kwa mapana. Si tu polisi hawaruhusiwi kukuweka ndani kwa makosa kama haya bali pia hawaruhusiwi hata kukuweka chini ya ulinzi. Kukuweka chini ya ulinzi ni kuzuia uhuru wako wa kutembea kwa namna yoyote ile, hata kwa kukwambia hapo ulipo usitoke.
Katika kesi ya Rudolf v Athumani (1982) TLR 100 mahakama ilisema kuwa ni kazi ya polisi pale wanapoletewa mashtaka kuchambua ikiwa mashtaka yaliyoletwa kwao ni madai au ni jinai ili ikiwa ni jinai wayachukue na ikiwa ni madai waachane nayo na wamshauri mleta mashtaka/malalamiko(informer) hatua sahihi za kuchukua.
Jaji Sammatta aliongeza kuwa polisi hawaruhusiwi kumweka mtu chini ya ulinzi kwa makosa ya madai.
Hivyo makala MAKALA SHERIA: POLISI HAWARUHUSIWI KUCHUKUA KESI ZA KUDAIANA HELA
yaani makala yote MAKALA SHERIA: POLISI HAWARUHUSIWI KUCHUKUA KESI ZA KUDAIANA HELA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKALA SHERIA: POLISI HAWARUHUSIWI KUCHUKUA KESI ZA KUDAIANA HELA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/makala-sheria-polisi-hawaruhusiwi.html
0 Response to "MAKALA SHERIA: POLISI HAWARUHUSIWI KUCHUKUA KESI ZA KUDAIANA HELA"
Post a Comment