title : WIZARA YA MAMBO YA NJE YAIKABIDHI TBA NYUMBA ZILIZOREJESHWA NA UMOJA WA ULAYA NCHINI
kiungo : WIZARA YA MAMBO YA NJE YAIKABIDHI TBA NYUMBA ZILIZOREJESHWA NA UMOJA WA ULAYA NCHINI
WIZARA YA MAMBO YA NJE YAIKABIDHI TBA NYUMBA ZILIZOREJESHWA NA UMOJA WA ULAYA NCHINI
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Mhe. Roeland van de Geer wakisaini Hati ya Makabidhiano ya nyumba nne (4) kutoka Umoja wa Ulaya zilizopo katika maeneo tofauti ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo zimekabidhiwa kwa Wizara na EU baada ya kutumiwa na Umoja huo tokea miaka ya 1975. Baada ya makabiadhiano hayo, Wizara ilizikabidhi nyumba hizo kwa Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA). Makabidhiano hayo yalifanyika Wizarani tarehe 11 Aprili, 2018.
Balozi Mushy kwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi. Elius Mwakalinga wakisaini hati ya makabidhiano kama ishara kwa Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuzikabidhi kwa TBA nyumba nne (4) zilizopokelewa na Wizara kutoka EU.
Balozi Mushy na Balozi Roeland van de Geer wakibadilishana hati hiyo baada ya kusaini
Balozi Mushy na Balozi van de Geer wakionesha hati hiyo .
Hivyo makala WIZARA YA MAMBO YA NJE YAIKABIDHI TBA NYUMBA ZILIZOREJESHWA NA UMOJA WA ULAYA NCHINI
yaani makala yote WIZARA YA MAMBO YA NJE YAIKABIDHI TBA NYUMBA ZILIZOREJESHWA NA UMOJA WA ULAYA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA MAMBO YA NJE YAIKABIDHI TBA NYUMBA ZILIZOREJESHWA NA UMOJA WA ULAYA NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/wizara-ya-mambo-ya-nje-yaikabidhi-tba.html
0 Response to "WIZARA YA MAMBO YA NJE YAIKABIDHI TBA NYUMBA ZILIZOREJESHWA NA UMOJA WA ULAYA NCHINI"
Post a Comment