title : WAZIRI KALEMANI AFUNGUA UMEME WA GRIDI NGARA
kiungo : WAZIRI KALEMANI AFUNGUA UMEME WA GRIDI NGARA
WAZIRI KALEMANI AFUNGUA UMEME WA GRIDI NGARA
Na Veronica Simba - Ngara
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amefungua matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu hivyo kuwezesha Wilaya hiyo kuachana na matumizi ya umeme wa mafuta.
Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi huo, Waziri Kalemani alisema kuwa yeye pamoja na watendaji wote wa Wizara na Taasisi zake hususan TANESCO na REA, wamedhamiria kutekeleza kwa vitendo, azma ya Rais John Magufuli ya kuhakikisha kunakuwepo na umeme wa uhakika nchini kote ili kuchochea uchumi wa viwanda.
“Serikali imekusudia kujenga uchumi wa viwanda na kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati. Hayo yote yanahitaji nishati ya uhakika, na ndicho tunachotekeleza.”
Alisema kuwa, mpango wa serikali ni kuiunganisha nchi nzima katika umeme wa Gridi ya Taifa ili wananchi wote wanufaike kwa kupata umeme wa aina moja.
Akifafanua Zaidi, Waziri kalemani alisema kuwa uunganishaji umeme wa Gridi ya Taifa umeshafanyika kutoka Mbagala Dar es Salaam kupitia Mkuranga, Kibiti, Ikwiriri, Utete, SomangaFungu hadi Lindi.
“Kwa sasa tunaendelea kuunganisha Lindi mpaka Mtwara ambapo kufikia mwisho wa mwezi huu, watanzania watakuwa wanatumia umeme wa Gridi ya Taifa kutoka pembe ya Kusini mwa nchi Mtwara hadi pembe nyingine ya nchi iliyopo Magharibi ambayo ni Ngara Kagera,” alisema.
Aidha, aliongeza kuwa, kazi iliyobaki ni kuunganisha upande mwingine wa nchi ambao unaanzia Mbeya kupitia Sumbawanga, Kigoma, Mpanda, Nyakanazi hadi Geita na Bulyanhulu. Alisema kazi hiyo inatarajiwa kukamilika ifikapo 2020/21.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha Mtambo maalum unaoruhusu kuwaka kwa umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, baada ya kuzima ule uliokuwa ukiwasha umeme wa mafuta ya dizeli, Aprili 8 mwaka huu.
Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (waliokaa-katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, TANESCO na REA baada ya hafla ya ufunguzi wa matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka (wa pili-kushoto) akimweleza jambo Mbunge wa Ngara, Alex Gashaza (kulia), wakati wakimsubiri Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kuwasili kwa ajili ya ufunguzi wa matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu. Wengine pichani ni viongozi mbalimbali kutoka wizarani, TANESCO na REA.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI KALEMANI AFUNGUA UMEME WA GRIDI NGARA
yaani makala yote WAZIRI KALEMANI AFUNGUA UMEME WA GRIDI NGARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KALEMANI AFUNGUA UMEME WA GRIDI NGARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/waziri-kalemani-afungua-umeme-wa-gridi.html
0 Response to "WAZIRI KALEMANI AFUNGUA UMEME WA GRIDI NGARA"
Post a Comment