title : Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushirikishwa katika Tuzo za The African Prestigious Awards
kiungo : Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushirikishwa katika Tuzo za The African Prestigious Awards
Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushirikishwa katika Tuzo za The African Prestigious Awards
Na Anitha Jonas – WHUSM
Utendaji uliyotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na ukuwaji wa sekta ya filamu nchini ndiyo vinavochangia kuitangaza nchi yetu katika tuzo za The African Prestious Awards.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana katika tuzo hizo.
“Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, napia tuna wasanii watatu ndani ya tansia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika,Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora Afrika,”alisema Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika sherehe hiyo ya kukabidhi bendera Mheshimiwa Mwakyembe aliwasisitiza wasanii wanchini kuendelea kuandaa kazi zinazoonyesha ubunifu wao kwani ukuaji wa tansia ya filamu Tanzania uko mikononi mwao na si vinginevyo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa jana jijini Dar es Salaam anayetarajia kwenda nchini Ghana mapema wiki hii katika tuzo za The African Prestigious Awards ambapo amechaguliwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika,wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akimkabidhi Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa tiketi ya ndege jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya safari yake ya kwenda nchini Ghana mapema wiki hii katika tuzo za The African Prestigious Awards ambapo amechaguliwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika,kutoka kulia wapili ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania Bw.Godfrey Mngereza.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo(wakwanza kushoto) akifafanua kwa waandishi wa habari na wadau wa sanaa (hawapo pichani) kuhusu tuzo za The Africa Prestigious Awards jana jijini Dar es Salaam zitakazotolewa nchini Ghana hivi karibuni kwa kueleza heshima ya tuzo hizo na Tanzania imepata heshima ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli nae kuteuliwa kuwania tuzo ya kiongozi bora Afrika,wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe.
Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa akiahidi kwa Waziri wa habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam katika sherehe ya kukabidhiwa bendera kuwa atarudi na tuzo hata kama yeye hatopata basi ataweza na kurudi na hata tuzo ya Msanii Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika au Tuzo ya Msanii King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika au Mpiga picha Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga picha Bora Afrika katika tuzo za The African Prestigious Awards zitakazotolewa nchini Ghana hivi karibuni,wa kwanza kulia ni Mama Mzazi wa Msanii Monalisa Bibi Suzan Lewis maarufu kama Natasha.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushirikishwa katika Tuzo za The African Prestigious Awards
yaani makala yote Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushirikishwa katika Tuzo za The African Prestigious Awards Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushirikishwa katika Tuzo za The African Prestigious Awards mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/rais-wa-jamhuri-ya-muungano-tanzania.html
0 Response to "Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushirikishwa katika Tuzo za The African Prestigious Awards"
Post a Comment