title : MAHAKAMA KISUTU YATAKA KILA CHOMBO KIHESHIMIWE
kiungo : MAHAKAMA KISUTU YATAKA KILA CHOMBO KIHESHIMIWE
MAHAKAMA KISUTU YATAKA KILA CHOMBO KIHESHIMIWE
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kila chombo kinapaswa kufanya kazi zake kwa kuheshimiana na haipendezi kila mara zitolewe amri ambazo hazitekelezwi.
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ameyasema hayo leo Aprili 11 mwaka wakati kesi ya utakatishaji wa fedha inayomkaboli mmiliki wa IPTL Harbinder Sethi na mwenzake, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutekeleza amri aliyoitoa ya kumpeleka mshtakiwa Sethi kutibiwa katika Hospital ya Taifa Muhimbili.
"Ninaamini, kila chombo kinapaswa kufanya kazi zake kwa kuheshimiana, haipendezi kila wakati tutoe amri ambazo hazitekelezwi, hivyo naamuru apelekwe hospital kinyume na hapo nitatoa amri nyingine kwa mujibu wa sheria,"amesema Hakimu Shaidi.
Mapema, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai mahakani hapo upelelezi wa kesi hiyo bado hujakamilika, pia wameshindwa kumpeleka Sethi hospital kwa sababu Sethi alihamishwa gereza kutoka Segerea kwenda Ukonga, pia alidai mshtakiwa aliomba daktari wake kutoka Afrika Kusini awepo wakati akipatiwa matibabu.
Wakili wa utetezi, Hajra Mungula alipinga vikali Hoja hizo na kudai kuwa hazina msingi kwa sababu Sethi hakuwahi kuzungumzia suala la daktari na kuongeza, kuwa katika gereza la Ukonga Sethi haruhusiwi kuonana na mtu yoyote hata mke wake wa ndoa.
Kutokana hoja hizo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 25 mwaka 2018.
Mbali ya Sethi, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya dola za Marekani USD 22, 198,544.60 na Sh.bilioni 309.
Hivyo makala MAHAKAMA KISUTU YATAKA KILA CHOMBO KIHESHIMIWE
yaani makala yote MAHAKAMA KISUTU YATAKA KILA CHOMBO KIHESHIMIWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA KISUTU YATAKA KILA CHOMBO KIHESHIMIWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mahakama-kisutu-yataka-kila-chombo.html
0 Response to "MAHAKAMA KISUTU YATAKA KILA CHOMBO KIHESHIMIWE"
Post a Comment