kesi inayowakabili vigogo wawili wa madini ya almasi yapigwa kalenda

kesi inayowakabili vigogo wawili wa madini ya almasi yapigwa kalenda - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa kesi inayowakabili vigogo wawili wa madini ya almasi yapigwa kalenda, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : kesi inayowakabili vigogo wawili wa madini ya almasi yapigwa kalenda
kiungo : kesi inayowakabili vigogo wawili wa madini ya almasi yapigwa kalenda

soma pia


kesi inayowakabili vigogo wawili wa madini ya almasi yapigwa kalenda

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Aprili 9, 2018 imeelezwa kuwa, jalaa la kesi inayowakabili vigogo wawili wa uthaminishaji wa madini ya almasi wa serikali,  akiwemo  Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (TANSORT), Archard Kalugendo, bado liko kwa DPP.

Wakili wa Serikali, Salim Msemo amemeeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbrad Mashauri, kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa, upelelezi bado haujakamilika. Kalugendo na mthamini almasi wa serikali, Edward Rweyemamu, walipanda kizimbani mahakamani hapo wakati shauri lilipopelekwa kwa kutajwa.

Msemo amedai jalada la kesi hiyo ambalo awali lilikuwa kwa DPP lilirudishwa kwa DCI ambaye ameshalifanyia kazi na limerudishwa tena kwa DPP na sasa  wanasubiri maelekezo ya DPP ili kesi iweze kuendelea.

Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai Novemba 9, mwaka jana, upande wa jamhuri ulieleza upelelezi umekamilika na Februari 27, mwaka huu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage baada ya kuonekana ucheleweshwaji wa kesi bila ya sababu ilitoa siku 14 ya kuiambia mahakama ni lini wataendelea na kesi hiyo. Ulidai hoja hizo wanaona zinazidi kuchelewesha kesi, hivyo upande wa jamhuri useme kwa nini amri halali ya mahakama haitekelezeki.

Wakili Msemo amedai ili kesi ianze kusikilizwa lazima mambo yote husika katika shauri hilo yawe yamekamilika na kukamilika kwa upelelezi hakuondoi yale yanayojitokeza na kustahili kufanyiwa kazi katika shauri hilo. Kufuatia hayo, kesi imeahirishwa hadi Aprili 23, mwaka huu, kwa kutajwa na washitakiwa walirudishwa mahabusu.

Washitakiwa hao ambao wako mahabusu wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia serikali hasara ya sh. bilioni 2.4. Kalugendo na Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini wanakabiliwa na shitaka la kuisababishia serikali hasara ya sh. 2,486,397,982.54, ambalo waliposomewa mara ya kwanza hawakutakiwa kujibu kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Washitakiwa hao wanadaiwa walitenda kosa hilo, kati ya Agosti 25 na 31, mwaka jana, katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga. Inadaiwa washitakiwa hao kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa serikali na waajiriwa wa wizara hiyo waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43 (sawa na sh. 2,486,397,982).


Hivyo makala kesi inayowakabili vigogo wawili wa madini ya almasi yapigwa kalenda

yaani makala yote kesi inayowakabili vigogo wawili wa madini ya almasi yapigwa kalenda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala kesi inayowakabili vigogo wawili wa madini ya almasi yapigwa kalenda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/kesi-inayowakabili-vigogo-wawili-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "kesi inayowakabili vigogo wawili wa madini ya almasi yapigwa kalenda"

Post a Comment