JUHUDI ZA TALGWU ZA KUTETEA WAFANYAKAZI ZA ZAAMATUNDA

JUHUDI ZA TALGWU ZA KUTETEA WAFANYAKAZI ZA ZAAMATUNDA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JUHUDI ZA TALGWU ZA KUTETEA WAFANYAKAZI ZA ZAAMATUNDA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JUHUDI ZA TALGWU ZA KUTETEA WAFANYAKAZI ZA ZAAMATUNDA
kiungo : JUHUDI ZA TALGWU ZA KUTETEA WAFANYAKAZI ZA ZAAMATUNDA

soma pia


JUHUDI ZA TALGWU ZA KUTETEA WAFANYAKAZI ZA ZAAMATUNDA


Pichani ni Katibu Mkuu wa chamaWafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) , Rashid Mohamed Mtima akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) leo Jijini dar es Salaam,kuzungumzia uamuzi wa serikali kuwarudisha kazini wafanyakazi wa darasa la saba(Picha Zote Na John Luhende) 

Mwambawahabari 
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimeipongeza  Serikali na wa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo bunge wa jimbo la Geita Mjini, Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma kwa uzalendo wake na kulifuatilia  suala la watumishi wa umma waliofukuzwa kazi wenye sifa ya darasa la saba, na mpaka serikali kuamua kuwarudisha kazini.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Rashid Mohamed  Mtima  wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari leo baada ya kupita siku moja tokea serikali ilivyotoa kauli yake kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika ya kuagiza watumishi wa umma 1,370 walioajiriwa kabla ya Mei 20, 2004 ambao hawakufaulu mtihani wa kidato cha nne, (darasa la saba) na waliondolewa kazini kwa kigezo cha vyeti vya kidato cha nne, warudishwe kazini mara moja na wapewe stahiki zao zote ikiwemo mishahara yao tangu walipoachishwa kazi.

"Suala hili sisi tumeanza muda mrefu kulihangaikia lakini'last week' tuliwaona wabunge walivyokuwa wamechachamaa Bungeni wakiongozwa na Mbunge wa jimbo la Geita Mjini, Joseph Kasheku Msukuma kwa kuweza kulipigia kelele jambo hili.... tunawashukuru sana, kwa maana hata kama lingekuwa lipo kwenye mchakato la kufanyiwa kazi lakini wao waliliongezea kazi zaidi mpaka serikali ikatangaza kuwarudisha kazini", amesema Mtima.

Pamoja na hayo, Mtima ameendelea kwa kusema "kwa niaba ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), napenda kutoa shukrani kwa serikali ya awamu ya tano kwa kuzingatia mapendekezo tuliyowasilisha serikalini Machi 22, 2018 na hatimaye jana yakafanyiwa kazi. 

"Kwa kweli jambo hili tunashukuru sana kwa maana serikali imekuwa sikivu. Pia tunapenda kutoa shukrani kwa Waziri Mkuu kwa namna alivyoweza kutusaidia kipindi tulivyokuwa tunahangaikia mchakato huu".

Kwa upande mwingine, Mtima amesema wanachama wake wamefurahishwa na uamuzi huo wa serikali kwa kuwa umeweza kurudisha matumaini mapya kwa watumishi hao waliofukuzwa kazi hapo awali.


Hivyo makala JUHUDI ZA TALGWU ZA KUTETEA WAFANYAKAZI ZA ZAAMATUNDA

yaani makala yote JUHUDI ZA TALGWU ZA KUTETEA WAFANYAKAZI ZA ZAAMATUNDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JUHUDI ZA TALGWU ZA KUTETEA WAFANYAKAZI ZA ZAAMATUNDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/juhudi-za-talgwu-za-kutetea-wafanyakazi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "JUHUDI ZA TALGWU ZA KUTETEA WAFANYAKAZI ZA ZAAMATUNDA"

Post a Comment