DC MJEMA ATOA TUZO KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO MTIHANI WA TAIFA 217.

DC MJEMA ATOA TUZO KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO MTIHANI WA TAIFA 217. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC MJEMA ATOA TUZO KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO MTIHANI WA TAIFA 217., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC MJEMA ATOA TUZO KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO MTIHANI WA TAIFA 217.
kiungo : DC MJEMA ATOA TUZO KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO MTIHANI WA TAIFA 217.

soma pia


DC MJEMA ATOA TUZO KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO MTIHANI WA TAIFA 217.

Mwambawahabari 
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema amekabidhi tuzo kwa shule za msingi zilizofanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2017 lengo likiwa ni kutoa motisha kwa walimu pamoja na wadau mbalimbali wa Elimu ili kuendelea kufanya vizuri zaidi.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo hizo jijini Dar es Salaam leo Dc Mjema amesema katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala katika maotokeo ya kumaliza elimu ya msingi za manispaa hiyo zimefanya vizuri ambapo katika wilaya hiyo ilishika nafasi ya nne (4) kimkoa na nafasi ya pili(2) katika Wilaya  na wameamua kutoa tuzo katika shule hizo ili kuongeza chachu ya kuongeza Ufaulu. 

Amesema tuzo hizo zitawasaidia kuwakumbusha kufanya vizuri ili kufikia nafasi ya kwanza kwa mkoa na kwa wilaya kwani miaka ya nyuma manispaa hiyo shule za msingi zilionekana kushika nafasi za mwisho.


"Tuzo hizi mnazozipata leo ziwe chachu ya kufanya vizuri zaidi na ziwe deni kwenu kuwakumbusha kuwa mnatakiwa kushika nafasi ya kwanza katika mkoa na hata katika Wilaya na hata wale watakaokosa tuzo msione wivu ila mjitahidi kufanya vizuri na ninyi mapate tuzo kama wanaopata leo" Amesema Mjema.
Aidha amebainisha kuwa jitihada za kuwezesha kufanya vizuri katika shule za msingi ni kutokana na ukaribu uliokuwepo kati ya walimu na wazazi ambapo walikuwa wakiwaita wazazi wa watoto wanaofanya vibaya ili kubaini nini tatizo na kupelekea wanafunzi kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.
Kwa Upande wake Afisa elimu msingi Elizabeth Thomas, amesema Idara ya elimu ya Msingi imelenga kutoa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE)  mwaka 2017 zenye lengo la kutoa motisha nakuwapongeza walimu kwa kazi kubwa ya ufundishaji na ujifinzaji waliofanya na kuzaa matunda ya matokeo mazuri.


Amesema Jumla ya shule 184, zikiwemo za Serikali 107 na zisizo za Serikali 77,ambapo jumla ya wanafunzi 21,704 walisajiliwa kufanya mtihani wakiwemo wavulana 10,270 na wasichana 11,434.

Aidha wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 21,569 wavulana 10,184 na wasichana 11,365 sawa na asilimia 99.3% waliofaulu ni wanafunzi 19,236 wakiwemo wavulana 9,199 na wasichana 10,037 sawa na asilimia 89% na wanafunzi wote hao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018.


Amebainisha kuwa tuzo hizo zimetolewa katika makundi mbalimbali zikiwemo shule  kumi bora,shule zilizopandisha ufaulu zaidi ukulinganishwa na ufaulu wa mwaka 2016, kata iliyofanya vizuri, shule zilizofanya mtihani  kwa Mara ya kwanza na zikafanya vizuri pamoja na kutoa tuzo maalumu kwa wadau mbalimbali.


Hivyo makala DC MJEMA ATOA TUZO KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO MTIHANI WA TAIFA 217.

yaani makala yote DC MJEMA ATOA TUZO KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO MTIHANI WA TAIFA 217. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC MJEMA ATOA TUZO KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO MTIHANI WA TAIFA 217. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/dc-mjema-atoa-tuzo-kwa-shule-za-msingi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DC MJEMA ATOA TUZO KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO MTIHANI WA TAIFA 217."

Post a Comment