title : BALOZI DKT. ABDALLAH SALEH POSSI AKUTANA NA WAFANYABISHARA WA POLAND WENYE NIA YA KUWEKEZA TANZANIA JIJINI WARSAW
kiungo : BALOZI DKT. ABDALLAH SALEH POSSI AKUTANA NA WAFANYABISHARA WA POLAND WENYE NIA YA KUWEKEZA TANZANIA JIJINI WARSAW
BALOZI DKT. ABDALLAH SALEH POSSI AKUTANA NA WAFANYABISHARA WA POLAND WENYE NIA YA KUWEKEZA TANZANIA JIJINI WARSAW
Mnamo April 24, 2018 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Poland, Dr. Abdallah Saleh Possi, alikutana na wadau mbalimbali wa uwekezaji katika mkutano wa kibiashara ulioandaliwa na jumuia ya biashara ya Poland. Mkutano huo ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya safari ya kibiashara inayotarajiwa kufanyika mwezi juni mwaka huu. Safari hiyo itahusisha wafanyabiashara kutoka Poland wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania.
Balozi aliwahimiza wafanyabiashara kutoka Poland kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali, haswa zinazotegemea mali ghafi kutoka nchini, na zenye uwezo wa kutengeneza ajira kwa wananchi wengi, na hivyo kupunguza utegemezi wa uagizaji bidhaa kutoka nje. Sekta hizo ni kama vile madawa, nguo, kilimo na chakula (hussusan uzalishaji wa sukari na mafuta ya kula). Pia balozi aliwahimiza wawekezaji hao kuangalia fursa katima sekta nyingine, haswa nishati mbadala na utalii.
Wahudhuriaji walionyesha kurishishwa na muelekeo wa uchumi wa Tanzania. Licha ya baadhi ya watoa mada kuainisha changamoto mbalimbali, mkutano huu ulitoa taswira ya kujengeka ushawishi miongoni mwa wafanyabiashara wa Poland kuhusiana na uwekezaji Afrika, haswa Tanzania.
Mada mbalimbali ziliwasilishwa na: Balozi Jerzy Drożdż, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kimataifa kutoka kutoka taasisi ya biashara ya Poland (Polish Chamber of Commerce); Bw. Eugeniusz Rzewuski, Kaimu Balozi wa zamani wa Poland nchini Tanzania; Balozi. Jan Wieliński, Balozi Mstaafu wa Poland katika nchi kadhaa za Afrika; Bw. Robert Zduńczyk, Rais wa Taasisi ya Uchumi Poland-East Africa; Bi, Agata Świtalska-Krych, Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo wa Wielkopolski, mfuko unaosaidia biashara ndogo na za kati, na maendeleo mijini; Bw. Konrad Pawlik, Makamu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Poland; Bi. Katarzyna Kwiecień, Mkurugenzi wa National Support Center for Agriculture; Bw. Wojciech Rząsiecki, Mkuu wa Idara ya Mikopo ya Serikali (Government Export Credits) Wizara ya Mambo ya Nje ya Poland; Bw. Łukasz Porażyński, kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Ujasiriamali na Teknolojia ya Poland; Bw. Piotr Maciaszek, mkurugenzi wa Export Credit Insurance Corporation Joint Stock Company (KUKE); Bw. Arkadiusz Zabłoński, Mkurugenzi wa Idara ya Kusaidia Biashara ya Mauzo ya Nje (Department of Export Support, BGK).
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Poland, Dr. Abdallah Saleh Possi, akibadilishana mawazo na wadau mbalimbali wa uwekezaji pembeni ya mkutano wa kibiashara ulioandaliwa na jumuia ya biashara ya Poland jijini Warsaw.
Wadau mbalimbali wa uwekezaji wa nchi ya Poland wakiwa kwenye mkutano wa kibiashara ulioandaliwa na jumuia ya biashara ya Poland jijini Warsaw uliohudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Poland, Dr. Abdallah Saleh Possi
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Poland, Dr. Abdallah Saleh Possi na ofisa wa ubalozi pamoja na viongozi wa wafanyabiashara kutoka Poland wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania.
Balozi Jerzy Drożdż, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kimataifa kutoka kutoka taasisi ya biashara ya Poland (Polish Chamber of Commerce) akitoa mada kwenye mkutano huo.
Hivyo makala BALOZI DKT. ABDALLAH SALEH POSSI AKUTANA NA WAFANYABISHARA WA POLAND WENYE NIA YA KUWEKEZA TANZANIA JIJINI WARSAW
yaani makala yote BALOZI DKT. ABDALLAH SALEH POSSI AKUTANA NA WAFANYABISHARA WA POLAND WENYE NIA YA KUWEKEZA TANZANIA JIJINI WARSAW Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI DKT. ABDALLAH SALEH POSSI AKUTANA NA WAFANYABISHARA WA POLAND WENYE NIA YA KUWEKEZA TANZANIA JIJINI WARSAW mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/balozi-dkt-abdallah-saleh-possi-akutana.html
0 Response to "BALOZI DKT. ABDALLAH SALEH POSSI AKUTANA NA WAFANYABISHARA WA POLAND WENYE NIA YA KUWEKEZA TANZANIA JIJINI WARSAW"
Post a Comment