title : WIZARA YA AFYA YATAJA SABABU ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME
kiungo : WIZARA YA AFYA YATAJA SABABU ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME
WIZARA YA AFYA YATAJA SABABU ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME
Said Mwishehe,Globu ya jamii
WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na
Watoto imetaja baadhi ya sababu zinazochangia
kupungua kwa nguvu za kiume kwa wanaume wengi
nchini.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto
Dk.Faustine Ndugulile amesema utafiti wa kisayansi
duniani unaonesha kuwapo kwa tatizo la nguvu za
kiume.
Amefafanunua kwa Tanzania hakuna utafiti rasmi
ambao umefanyika kubaini tatizo hilo la upungufu wa
nguvu za kiume nchini kwetu na kueleza ipo haja ya
kufanya angalau utafiti ili kubaini udogo au ukubwa
wa tatizo hilo.
Ametaja baadhi ya sababu zinazochangia tatizo la
ukosefu wa nguvu za kiume ni
ulaji wa vyakula vya mafuta, kutofanya mazoezi,
matumizi ya ulevi wa pombe pamoja na uvutaji
sigara.
"Hizo ni miongoni mwasababu ambazo kwa kiasi
kikubwa zinaweza kusababisha mwanaume kuwa na
tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume.Hivyo tunashauri
kwenye chakula ule chakula bora na si bora
chakula,"amesema Dk.Ndugulile.
Ameeleza Serikali haijawekeza kwenye afya ya uzazi
kwa wanaume bali imejikita zaidi kwenye afya ya
uzazi kwa wanawake.
Ameweka wazi ukiangalia takwimu ya uzazi na akina
mama kujifungua Tanzania haina shida lakini taarifa
za kisayansi duniani zinaeleza kuna tatizo la ukosefu
wa nguvu za kiume duniani.
Dk.Ndugulile amesema kwenye aina ya dawa tano
ambazo zimesajiliwa na Baraza la tiba asili na tiba
mbadala kuna dawa inaitwa Ujana ambayo
inahusika na mambo hayo ya upungufu wa nguvu za
kiume.
Pia amesema tayari Taasisi ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu(NIMR), nayo kuna dawa
wanaendelea kuifanyia utafiti na watakapokamilisha itaingia kwenye matumizi.
Hivyo makala WIZARA YA AFYA YATAJA SABABU ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME
yaani makala yote WIZARA YA AFYA YATAJA SABABU ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA AFYA YATAJA SABABU ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/wizara-ya-afya-yataja-sababu-za-ukosefu.html
0 Response to "WIZARA YA AFYA YATAJA SABABU ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME"
Post a Comment