UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo

UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo
kiungo : UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo

soma pia


UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo

UMOJA wa Mataifa umeingia makubaliano ya kuimarisha upatikanaji na usambazaji wa habari za maendeleo na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO).

Makubaliano hayo yamelenga kuimarisha upatikanaji na utoaji habari wa pamoja kuhusu mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa serikali na malengo ya maendeleo endelevu ya dunia.

Kwa mujibu Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez  makubaliano hayo yatachagiza kupatikana kwa habari kuhusiana na utekelezaji  wa malengo ya maendeleo endelevu unaokwenda sambamba na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa Tanzania.

Akizungumzia malengo hayo kwa maofisa wa mawasiliano wa serikali wanaokutana mjini Arusha kwa semina ya wiki moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya TAGCO na Wizara ya Habari na kufadhiliwa na Umoja wa Mataifa, alisisitiza kuwa malengo hayo yanahitaji kuwasilishwa kwa wananchi na pia kupigiwa chapuo.
 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akiwasilisha mada kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia na uhusiano wake na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wakati wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea Jijini Arusha.
Ofisa Habari wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru akiuliza namna ambavyo mapambano dhidi ya rushwa yanavyoweza kuwa sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi Suzan Mlawi (kulia) wakifuatilia mada kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia na uhusiano wake na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wakati wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea Jijini Arusha.
 Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Maelezo Dk. Hassan Abbas akizungumza  na waandishi wa habari nje wakati wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea Jijini Arusha.
Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakifuatilia mada kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia na uhusiano wake na mpango wa maendeleo wa miaka mitano ikiwasilishwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez hayupo pichani katika mkutano huo wa 14 unaoendelea jijini Arusha.



Hivyo makala UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo

yaani makala yote UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/un-waingia-makubaliano-na-serikali.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo"

Post a Comment