TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI

TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI
kiungo : TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI

soma pia


TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), kuhakikisha inatatua changamoto zote zinazokwamisha mradi wa ujenzi wa gati mpya.

Prof. Marawa ametoa kauli hiyo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Gati mpya inayojengwa Mkoani Mtwara kwa ubia wa kampuni mbili za Kichina za China Railways Major Bridges Engineering Group Co. Ltd (CRMBEG) na China Railways Construction Engineering Group (CRCEG) na kubaini mapungufu katika utekelezaji wa mradi huo.

“Hatuwezi kuendelea kuchelewesha mradi huu muhimu kwa wakazi wa Mtwara, wakati fedha zipo na mikataba imeshasainiwa, naiagiza TPA kuhakikisha kuwa inatatua changamoto hizo na kuzitafutia ufumbuzi ndani ya miezi mitatu ili mradi ukamilike kwa wakati,” amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa miradi inayotekelezwa na Wakandarasi wazawa chini ya usimamizi wa TPA isimamiwe kwa kuzingatia viwango na muda uliopangwa na kuahidi kurejea baada ya miezi mitatu kukagua maendeleo ya miradi hiyo.
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali akiwasilisha taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Hayupo Pichani), kuhusu mapato na matumizi ya bandari hiyo, wakati Waziri huyo alipotembelea bandari hiyo kukagua maendeleo ya mradi wa gati.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiangalia eneo ambalo linajengwa maegesho ya kawaida ya mizigo katika bandari ya Mtwara, alipotembelea bandari hiyo kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika bandari hiyo.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya mradi wa Gati katika bandari ya Mtwara. Gati hiyo yenye urefu wa mita 300 inatarajiwa kukamilika mwaka 2019 na upanuzi wake utagharimu kiasi cha shiliingi zaidi ya bilioni 100.
Mhandisi wa Bandari ya Mtwara, Eng. Twaha Msita ambaye ni (katikati), akimwonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), ramani ya eneo la mradi wa kuegesha mizigo ya kawaida, alipokagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika bandari ya Mtwara. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Karim Mattaka.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Eng. Karim Mattaka (kushoto), alipokagua maendeleo ujenzi wa gati, Mkoani Mtwara.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/s Dott Services ltd (kushoto), anaejenga Barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50, alipokagua maendeleo ya ujenzi wake mkoani Mtwara. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoani Mtwara, Eng Dotto Chacha. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini Bw. Evod Mmanda.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiongea na wakazi wa Nanguruwe Mkoani Mtwara alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha Lami.



Hivyo makala TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI

yaani makala yote TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/tpa-mtwara-wapewa-miezi-mitatu-kutatua.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TPA MTWARA WAPEWA MIEZI MITATU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA GATI"

Post a Comment