title : TBA WATAKIWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UKARABATI WA MADARASA KATIKA SEKONDARI YA MILAMBO.
kiungo : TBA WATAKIWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UKARABATI WA MADARASA KATIKA SEKONDARI YA MILAMBO.
TBA WATAKIWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UKARABATI WA MADARASA KATIKA SEKONDARI YA MILAMBO.
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
SERIKALI imeitaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoani Tabora kuhakikisha wanatumia utaratibu ule EP4R wa kujenga chumba cha darasa kwa shilingi milioni 20 wakati wanafanya tathimini gharama halisi zitakazotumika katika ukarabati madarasa wanne na ujenzi wa chumba kimoja katika Sekondari ya Milambo ili kusaidia katika kupunguza gharama waliziweka hivi sasa.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Tabora na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa majengo katika Chuo cha Ualimu Tabora na Milambo Sekondari.
Alisema kuwa hakubaliani kutaka kutumia milioni 100 katika ukarabati wa vyumba vya madarasa vinne na ujenzi wa kimoja kwa gharama hiyo kwani ni kubwa mno.
Naibu Waziri huyo alisema wamekuwa wakitumia mpango EP4R ambapo shilingi milioni 20 zimeweza kujenga na kukamilisha darasa zuri likiwa na miundombinu pamoja na madawati ya wanafunzi na meza na kiti cha Mwalimu.
Alisema madarasa yanayotakiwa kukarabatiwa sio mabovu sana ni vema wakapunguza gharama ili hatimaye wakajikuta wametumia fedha ambazo hawawezi kuzitolea maelezo.
Aidha Naibu Waziri huyo aliwapongeza TBA kwa kukarabati vizuri mabweni matatu ya wanafunzi kwa shilingi milioni 255 na kuongeza kuwa kazi iliyofanyika ni nzuri na inaridhisha.
Awali Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Tabora Wencelaus Kizaba alisema tathimini ya awali iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Ardhi ilionyesha kuwa madarasa yote yangekarabatiwa kwa milioni 20 ambapo baada ya wao kupitia waliona fedha hizo zisingesaidia kutokana na shughuli za ukarabati ambayo inatakiwa kufanyika pale.
Alisema hali ya madarasa ilivyo yanahitaji kuinuliwa juu ili kuepusha maji yasiingie madarasani na kuweka na kuweka mabati mapya kwenye yale mabovu na ujenzi wa chumba kipya cha darasa.
Kizaba alisema kwa fedha zilizotengwa kwa shughuli hiyo zisingeweza kufanya chochote zaidi ya kuishia katika upakaji wa rangi huku maji yakiendelea kuingia darasa na baadhi ya sehemu za madarasa kuvuja.
Alisema kutokana kutofanywa kwa umakini na kuacha baadhi ya maeneo kuingizwa katika mradi wa ukarabati ndio maana hata katika ukarabati wa mabweni kumekuwepo na ongezeko la milioni 45 toka zile zilizotathiminiwa na Chuo Kikuu cha Ardhi za milioni 210.
Hivyo makala TBA WATAKIWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UKARABATI WA MADARASA KATIKA SEKONDARI YA MILAMBO.
yaani makala yote TBA WATAKIWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UKARABATI WA MADARASA KATIKA SEKONDARI YA MILAMBO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TBA WATAKIWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UKARABATI WA MADARASA KATIKA SEKONDARI YA MILAMBO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/tba-watakiwa-kupunguza-gharama-za.html
0 Response to "TBA WATAKIWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UKARABATI WA MADARASA KATIKA SEKONDARI YA MILAMBO."
Post a Comment