MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE

MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE
kiungo : MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE

soma pia


MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE


Na Yusuph Mussa, Korogwe.

BWENI la Mapinduzi la wanafunzi wa kidato cha pili na nne katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe limeteketea kwa moto, huku mali zote za wanafunzi ikiwemo fedha zimeungua.

Moto huo ulioanza 3.15 usiku jana Machi 4, 2018, uliwakuta wanafunzi 43 wa bweni hilo wote wakiwa darasani (prepo), hivyo mali zao zote kuanzia vitanda 19 vya kulala wanafunzi wawili wawili na vitanda vitano vya kulala mtu mmoja vimeteketea kwa moto.

Akisoma taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela, Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Rehema Bwasi, alisema mali nyingine zilizoteketea ni magodoro 43, ambapo kati yao 26 ni ya shule na 17 ya wanafunzi. Pia vyandarua 43, shuka 86, blanketi 43, masanduku ya bati 43, mabegi 43 na fedha taslimu za wanafunzi mmoja mmoja sh. 336,500.

"Vitu vingine vilivyoungua ni pamoja na nguo za wanafunzi, miswaki, sabuni, vikombe, sahani pamoja na vitabu vya wanafunzi na vya shule. Ila tathmini inaendelea ili kuweza kujua hasara iliyotokana na moto huo" alisema.

Bwasi alisema kutokana na kadhia hiyo, baadhi ya wanafunzi walipata mshtuko, huku wengine wakiwa na magonjwa mbalimbali kama pumu na kifua, hivyo wanafunzi 41 walipelekwa Hospitali ya Wilaya na saba Zahanati ya Majengo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela(mwenye shati jeupe) akiangalia athari zilizosababishwa na moto ulioteketeza bweni katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe, Wilaya ya Korogwe. moto huo ulizuka usiku wa kuamkia leo, juu pichani akiwa ndani ya Bweni hilo linaloitwa Mapinduzi lililoteketea kwa moto. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Anisia Mauka. (Picha zote na Yusuph Mussa)
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela leo Machi 5, 2018 alifika Wilaya ya Korogwe kuangalia athari za moto Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe. Pichani akimfariji mmoja wa wanafunzi waliopata mkasa wa kuunguliwa na bweni la shule hiyo. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela leo Machi 5, 2018 alifika Wilaya ya Korogwe kuangalia athari za moto Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe. Pichani akimfariji mmoja wa wanafunzi waliopata mkasa wa kuunguliwa na bweni la shule hiyo. Kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said.
Bweni la Mapinduzi la Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe ambalo limeteketea kabisa kwa moto jana usiku Machi 4, 2018. Bweni hilo walikuwa wanalala wanafunzi 43 wa kidato cha pili na nne.



Hivyo makala MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE

yaani makala yote MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/moto-ulivyoteketeza-bweni-la-wasichana.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE"

Post a Comment