title : MBUNGE ROSE TWEVE ACHANGIA MAENDELEO YA UWT MKOA WA IRINGA
kiungo : MBUNGE ROSE TWEVE ACHANGIA MAENDELEO YA UWT MKOA WA IRINGA
MBUNGE ROSE TWEVE ACHANGIA MAENDELEO YA UWT MKOA WA IRINGA
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiongea wakati wa baraza la (UWT) manispaa ya Iringa lililofanyika katika ukumbi wa sabasaba mkoani Iringa na kusistiza wakipewa mitaji kutoka kwenye mfuko wake wanapaswa kuutunza mtaji huo ili uongeze faida.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve amewainua wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) kwa kutoa mitaji kupitia mfuko ambao ameuanzisha wa kuwainua wanawake wenye kipato kidogo.
Akizungumza nablog hii mbunge Tweve alisema kuwa lengo la kutoa mitaji hiyo ni kuwakomboa wanawake ambao wamekuwa wakisumbuka kufanya biashara ndogo ndogo ambazo ndio zimekuwa zikiendesha maisha yao.
“Mara kwa mara nimekuwa nikiwaona wanawake wengi wakiwa wanauza matunda,karaka na vitu vingine mitaani lakini mitaji yao ni midogo mno hivyo nikaamua kuanza kuwapatia mitaji kupitia mfuko wangu binafsi kwa wanawake wa wilaya ya Mufindi” alisema Tweve
Tweve alisema kuwa atahakikisha kuwa mfuko huo unakuwa mkombozi kwa wanawake wote wa mkoa wa Iringa kwa kuwa ameutengenezea malengo ambayo yameanza kuleta matunda kwenye wilaya ya mufindi na kusaidia kukuza mitaji ya wananchi na kuukuza mfuko pia.
“Matunda yameanza kupatikana kutokana nakuona faida ambayo imeanza kupatikana kwa wanawake ambao nilishawapa mitaji na mitaji hiyo imeanza kuleta faida ambapo sasa itakuwa fursa kwa wanawake wengi nao kupewa mitaji” alisema Tweve
Aidha mbunge Rose Tweve alimshukuru mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas kwa kuchangia mfuko kwa kuahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni hamsini na tatu (53,000,000) kwenye kata mia moja na sita (106) za mkoa wa Iringa.
“Kutoa kiasi ccha shilingi milioni hamsini na tatu (53,000,000) kwenye kata mia moja na sita (106) za mkoa wa Iringa sio kazi ndogo hivyo inapaswa kuzitumia pesa hizo pindi watakapo anza kutoa kama mitaji kwa wanawake wa mka wa Iringa” alisema Tweve
Lakini pia Tweve aliwaomba wanawake wanapewa mitaji hiyo kuitumia vizuri ili kuongeza faida ya mitaji yao pamoja na kuongeza idadi ya wanawake watakaopewa tena mitaji hiyo.
Hivyo makala MBUNGE ROSE TWEVE ACHANGIA MAENDELEO YA UWT MKOA WA IRINGA
yaani makala yote MBUNGE ROSE TWEVE ACHANGIA MAENDELEO YA UWT MKOA WA IRINGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE ROSE TWEVE ACHANGIA MAENDELEO YA UWT MKOA WA IRINGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mbunge-rose-tweve-achangia-maendeleo-ya.html
0 Response to "MBUNGE ROSE TWEVE ACHANGIA MAENDELEO YA UWT MKOA WA IRINGA"
Post a Comment