MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC

MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC
kiungo : MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC

soma pia


MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga Mary Chatanda amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Jumanne Shauri kupeleka wakaguzi kwenye Shule ya Sekondari Joel Bendera iliyopo Kijiji cha Kwakombo, Kata ya Kwamsisi.

Ni kutaka kubaini ukweli kuhusu matumizi ya fedha baada ya sh. milioni 150 zilizopelekwa shuleni hapo kumalizika, kabla ya ujenzi wa mabweni mawili kumalizika, huku tena zikihitajika sh. milioni 17 kumalizia ujenzi huo.

Chatanda alibaini hilo baada ya Machi 3, 2018 kufanya ziara kata ya Kwamsisi, na kusomewa taarifa na Mkuu wa Shule hiyo Nasson Msemwa kudai sh. milioni 150 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kujenga mabweni hayo ikiwa ni pamoja na kuweka samani, fedha zake zimekwisha.

“Mheshimiwa Mbunge, Serikali ilituletea sh. milioni 230, ambapo sh. milioni 150 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya wasichana na wavulana na sh. milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya manne. Fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ambapo tupo kwenye hatua za mwisho zimekwisha. Na ili tukamilishe mabweni hayo kunahitajika sh. milioni 17.

“Kwa upande wa ujenzi wa madarasa manne, bado tunakwenda vizuri, kwani pamoja na ujenzi kuwa kwenye hatua za mwisho, bado tuna sh. milioni 28” alisema Msemwa.
Mbunge wa Korogwe Mjini Mary Chatanda (wa tatu kulia) akisikiliza taarifa inayosomwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Joel Bendera Nasson Msemwa (wa pili kushoto). Hapo ndipo Chatanda aliliamsha ‘dude’ kutaka kujua kwa nini sh. milioni 150 zimeshindwa kukamilisha mabweni mawili.Yussuph Mussa, Korogwe
Madarasa mapya manne ya Shule ya Sekondari Joel Bendera, Kijiji cha Kwakombo, Kata ya Kwamsisi, Halmashauri ya Mji Korogwe. Madarasa hayo ambayo yapo kwenye hatua za mwisho kukamilika, Serikali ilitenga sh. milioni 80 kujenga madarasa hayo. (Picha na Yusuph Mussa).
Moja ya mabweni yaliyopo Shule ya Sekondari Joel Bendera Kijiji cha Kwakombo, Kata ya Kwamsisi, Halmashauri ya Mji Korogwe. Mabweni mawili yaliyojengwa shule hiyo, kila moja litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kwa wakati mmoja.PICHA ZOTE NA YUSSUPH MUSSA



Hivyo makala MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC

yaani makala yote MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mbunge-chatanda-ataka-ukaguzi-tsh.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MBUNGE CHATANDA ATAKA UKAGUZI TSH. MILIONI 230, UJENZI SHULE YA JOEL BENDERA SEC"

Post a Comment