MAKONDA AMSINDIKIZA AHAMED ALBAITY KUTIBIWA UCHINA

MAKONDA AMSINDIKIZA AHAMED ALBAITY KUTIBIWA UCHINA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKONDA AMSINDIKIZA AHAMED ALBAITY KUTIBIWA UCHINA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKONDA AMSINDIKIZA AHAMED ALBAITY KUTIBIWA UCHINA
kiungo : MAKONDA AMSINDIKIZA AHAMED ALBAITY KUTIBIWA UCHINA

soma pia


MAKONDA AMSINDIKIZA AHAMED ALBAITY KUTIBIWA UCHINA






 Rc Makonda akimkabidhi tiketi nne,mmoja wa ndugu anayesafiri na Ahamed

Mwambawahabari
 Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  leo amemtakia matibabu mema mwananchi Ahmed Albaity anayekwenda nchini China kutibiwa tatizo la uti wa mgongo ambalo amekuwa akisumbuliwa  nalo kwa takribani miaka kumi na moja akiwa kitandani na kuwataka wananchi kuendelea kumwombea ili aweze kufanikiwa katika matibabu yake.

Makonda ameyasema hayo leo wakati akimsindikiza  Ahmed Albaity  katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kutoa wito kwa watanzania wote kuendelea kumwombea na kuonyesha upendo kwake ili matibabu atakayopatiwa yaweze kwenda vizuri na kuweza kurejea katika hali iliyo nzuri.

"Wito wangu kwa watanzania wote ni kuendelea kumwombea ili dawa atakayoipata aweze kurejea katika hali yake hata kama siyo kupona kabisa basi tuweze kuona matokeo ya matibabu hayo"

Aidha Rc Makonda  amemtia moyo na kumtakia kila laheri katika matibabu yake na kumwambia Mungu amtangulie na kumtaka kutokakata tamaa kwani ataendelea kuwa pamoja naye siku zote.

Gharama za usafiri, fedha ya matumizi pamoja matibabu zimegaharimu  dola 52, ambazo ni zaidi ya million 107.

"Nafasi ya Ukuu wa Mkoa sio yangu bali ni ya watu na watu  na wana changamoto zao hivyo tunalazimika kutoka kwenda kuona mahitaji ya wananchi na hatimae waone thamani ya uongozi na Serikali yao, hatuna bajeti lakini Mimi kama Makonda niliniliona vyema niwatafute Marafiki zangu ili tumsaidie ndugu yetu Ahmed apate matibabu na kurejesha tabasamu, ninayo furaha kusema tumefanikiwa kupata Dola 52,000 sawa na zaidi ya Million 107" Alisema Makonda.

Pia amewashukuru wadau waliojitokeza kumchangia Ahamed kwani wameonyesha upendo mkubwa na kuwasii waendelee na moyo huo katika kuwasaidia wahitaji mbalimbali katika mkoa huo.

Kwa Upande wake Ahamed Albaity amemshukuru Rc MAKONDA pamoja na Rais John Pombe Magufuli kumchagua kuwa mkuu wa mkoa ambae anaguswa na matatizo ya wananchi na kumwomba aendelee na moyo huo huo katika kuwasaida wahitaji mbalimbali wanaofika kwake kuomba Msaada.

Aidha amesema wana Dar es salaam wanapaswa kujivunia kupata bahati ya kipekee ya kuwa na kiongozi imara anaejali wananchi wake pasipokujali Dini wala kabila.

Naye Farough Baghorah ambaye alikuwa mweka hazina amemshukuru Rc Makonda na kusema moyo aliouonyesha ni wa kipekee sana ambapo ameweza kumsadia na kufanikisha Ahamed Albaity kwenda kutibiwa nchini China ambaye ameteseka kwa takribani miaka kumi na moja, na sasa anakwenda kutibiwa na kwamba wataendelea kumwombea .


Hivyo makala MAKONDA AMSINDIKIZA AHAMED ALBAITY KUTIBIWA UCHINA

yaani makala yote MAKONDA AMSINDIKIZA AHAMED ALBAITY KUTIBIWA UCHINA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA AMSINDIKIZA AHAMED ALBAITY KUTIBIWA UCHINA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/makonda-amsindikiza-ahamed-albaity.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAKONDA AMSINDIKIZA AHAMED ALBAITY KUTIBIWA UCHINA"

Post a Comment