title : MAKALA YA SHERIA: KUPOTELEWA NA NYARAKA INAYOHITAJIKA MAHAKAMANI KAMA USHAHIDI
kiungo : MAKALA YA SHERIA: KUPOTELEWA NA NYARAKA INAYOHITAJIKA MAHAKAMANI KAMA USHAHIDI
MAKALA YA SHERIA: KUPOTELEWA NA NYARAKA INAYOHITAJIKA MAHAKAMANI KAMA USHAHIDI
Na Bashir Yakub.
Inaweza kuwa nyaraka muhimu kama hati ya nyumba, mkataba wa mauziano au mkataba mwingine wowote, wosia, kadi ya gari au ya mashine yoyote,hati ya kusimamia mirathi, cheti cha ndoa au vyeti vinginevyo, na nyaraka nyingine mbalimbali.
Nyaraka hii inaweza kuwa inatakiwa sehemu muhimu kama mahakamani ili kuthibitisha shauri au kesi yako. Na inaweza ikawa ni nyaraka ambayo kuwepo kwake ndio kushinda kwako na kutokuwepo kwake ndio kushindwa kwako.
Pamoja na umuhimu wa nyaraka hii bado umeitafuta kote pa kutafuta na hukuweza kuipata. Au hukuitafuta madhali tu unajua ilishapotea au iko mikononi mwa mtu ambaye hujui alipo na hawezi kupatikana. Katika mazingira ya namna hiyo makala yataeleza vitu vichache vinavyoweza kusaidia kutoka Sura ya sita,Sheria ya Ushahidi.
1. USHAHIDI WAKO.
Kitu kikubwa kinachomsaidia mtu kushinda kesi mahakamani ni ushahidi. Kadhalika kushindwa kwako pia ni ushahidi. Ukisema hiki kiwanja au nyumba ni yangu unatakiwa kuonesha hati au mkataba wa mauziano au vyote viwili.
Ukisema hili gari ni langu kadhalika uoneshe kadi yenye jina lako ama vinginevyo. Ukisema nilikuwa na ndoa halali uoneshe cheti cha ndoa ama vinginevyo. Ukisema nilimuuzia au kununua kitu fulani uoneshe mkataba ama risiti,vivyo hivyo nk, nk.
Hakimu au Jaji si mtu ambaye anakuwa eneo la tukio na hivyo kuwa katika nafasi ya kujua nini kilitokea huko. Yeye hajui chochote kilichotokea na hivyo taarifa zote anazipata kwenu mnaoshitakiana. Kwa msingi huu yupo katika wakati mgumu kuamua nani yuko sahihi na nani hayuko sahihi kwa kitu ambacho hakushuhudia na hakijui.
Kama hivi ndivyo kitu pekee cha kumuongoza hakimu/jaji huyu ambaye hakuwepo wakati mnadhulumiana, ni ushahidi wa kila mmoja atakaowasilisha. Hataangalia suraya mtu, kulia machozi kwa mtu, kuongea kwa kujiamini au kwa unyonge kwa mtu, umri wa mtu, rangi ya mtu,wala jinsia, bali ushahidi ulio uliowasilishwa na mtu.
Hivyo makala MAKALA YA SHERIA: KUPOTELEWA NA NYARAKA INAYOHITAJIKA MAHAKAMANI KAMA USHAHIDI
yaani makala yote MAKALA YA SHERIA: KUPOTELEWA NA NYARAKA INAYOHITAJIKA MAHAKAMANI KAMA USHAHIDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKALA YA SHERIA: KUPOTELEWA NA NYARAKA INAYOHITAJIKA MAHAKAMANI KAMA USHAHIDI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/makala-ya-sheria-kupotelewa-na-nyaraka.html
0 Response to "MAKALA YA SHERIA: KUPOTELEWA NA NYARAKA INAYOHITAJIKA MAHAKAMANI KAMA USHAHIDI"
Post a Comment