title : MADIWANI WA UYUI WAPITISHA BILIONI 1.9 KWA AJILI RZUKU YA MIUNDOMBINU
kiungo : MADIWANI WA UYUI WAPITISHA BILIONI 1.9 KWA AJILI RZUKU YA MIUNDOMBINU
MADIWANI WA UYUI WAPITISHA BILIONI 1.9 KWA AJILI RZUKU YA MIUNDOMBINU
NA TIGANYA VINCENT
RS-TABORA
Mwambawahabari
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Tabora-Uyui limepitisha mapendekezo ya marekebisho ya bajeti ya ruzuku ya miundombinu LGCDG ya bilioni 1.9 kwa ajili ya mwaka huu wa fedha (207/18).
Mapendekezo ya marekebisho ya bajeti hiyo yaliwasilishwa jana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Hadija Makuwani katika kikao cha dharura cha Baraza hilo.
Alisema wameamua kufanyika marekebisho hayo kufuatia agizo la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa za kuzitaka Halmashauri zote nchini kufanyia uchambuzi upya bajeti za miradi ili kuwa na michache inayotekelezeka na kukamilika kwa wakati na kwa asilimia 100.
Makuwani aliongeza miradi iliyopitishwa baada ya marekebisho ni pamoja na ujenzi wa madarasa 13 na majengo ya utawala matatu katika shule za Sekondari 6 ambayo itagharimu milioni 365.
Miradi mingine ni ujenzi wa nyumba mbili za walimu katika shule za Sekondari Usagari na ujenzi wa mabweni matano katika Shule za Sekondari ambayo itagharimu milioni 235.
Alitaja miradi mingine kuwa ni ukamilishaji wa vyumba 10 vya mahabara katika Sekondari 10 ambapo wanatarajia kutumia milioni 302.5.
Makuwani alisema pia kutakuwepo na ujenzi wa madarasa 11 na ofisi za walimu 4 katika shule za msingi ambao utagharimu milioni 190.
Mradi mwingine ni ukamamilishaji wa jengo la wagonjwa wan je (OPD) na ujenzi wa wodi mbili za wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ambapo watatumia milioni 300.
Makuwani alisema sehemu ya fedha hizo zitasaidia katika kukamilisha Zahanati ya Ishihimulwa ambapo milioni 70 zitatumika na ukamilishaji wa wodi ya wazazi katika Zahanati ya Imalakaseko kwa milioni 80.
Fedha nyingine jumla milioni 300 zitatumika kwa ajili ya kununulia nyumba za Shirika la Nyumba kwa ajili ya watumishi kuishi watumishi wa Halmashauri hiyo.
Makuwani alisema uratibu na ufuatiliaji utatumia milioni 96.9.
Hivyo makala MADIWANI WA UYUI WAPITISHA BILIONI 1.9 KWA AJILI RZUKU YA MIUNDOMBINU
yaani makala yote MADIWANI WA UYUI WAPITISHA BILIONI 1.9 KWA AJILI RZUKU YA MIUNDOMBINU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MADIWANI WA UYUI WAPITISHA BILIONI 1.9 KWA AJILI RZUKU YA MIUNDOMBINU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/madiwani-wa-uyui-wapitisha-bilioni-19.html
0 Response to "MADIWANI WA UYUI WAPITISHA BILIONI 1.9 KWA AJILI RZUKU YA MIUNDOMBINU"
Post a Comment