AJALI YA BASI NEW FORCE NA BASI DOGO TOYOTA HIACHE YASABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA KUJERUHI TISA KULAZWA WODINI HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO

AJALI YA BASI NEW FORCE NA BASI DOGO TOYOTA HIACHE YASABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA KUJERUHI TISA KULAZWA WODINI HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AJALI YA BASI NEW FORCE NA BASI DOGO TOYOTA HIACHE YASABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA KUJERUHI TISA KULAZWA WODINI HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AJALI YA BASI NEW FORCE NA BASI DOGO TOYOTA HIACHE YASABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA KUJERUHI TISA KULAZWA WODINI HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO
kiungo : AJALI YA BASI NEW FORCE NA BASI DOGO TOYOTA HIACHE YASABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA KUJERUHI TISA KULAZWA WODINI HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO

soma pia


AJALI YA BASI NEW FORCE NA BASI DOGO TOYOTA HIACHE YASABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA KUJERUHI TISA KULAZWA WODINI HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO

Na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro
WATU watano wakiwemo wanawake wanne na mwanaume mmoja ambaye ni dereva basi ndogo aina ya Toyota Hiache yenye namba za usajili T 962 BSE aliyetambuliwa kwa jina la Jackson Adam wamefariki dunia papo hapo baada yakugongana na basi  la  New force New lenye namba T 346 DLY likitokea  Dar es Salaam kuelekea Tunduma na kusababisha majeruhi  ya watu wengine tisa na kulazwa  hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibisha kutokea kwa ajali hiyo  Machi 4, mwaka huu majira ya saa nne asubuhi  katika barabara kuu ya Morogoro – Iringa  eneo la Lungemba – Rombo , Manispaa ya Morogoro kwa kuhusisha basi la aina ya Youtong  lenye namba za usajili T 346 DLY mali ya kampuni ya New force.
Basi hilo lilikuwa likitokea   Dar es Salaam kwenda Tunduma  na lilipofika eneo hilo liligongana uso kwa uso na basi ndogo  aina ya Toyota Hiache yenye namba za usajili T 962 BSE iambayo lilikuwa likitokea kijiji cha   Mlali, katika wilaya ya Mvomero kwenda Morogoro Mjini.
Kamanda Matei alisema katika ajali hiyo  abiria  watano waliokuwa ndani ya Toyota Hiache walifariki dunia papo hapo na wengine  tisa kujeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Morogoro  kwa ajili ya kupatiwa matibabu na hakukuwa na majeruhi kutoka  basi la New Force .
Kamanda wa Polisi wa huyo aliwataja waliofariki dunia ni pamoja na dereva wa basi dogo  Jackson Adam ambaye ni mkazi wa Kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro,  na wengine wanawake Georgina Aloyce (35) , Revocatha Raymond Lyimo , Mangasa Almasi  na Witness Leonard Mwamuni (26).
Pia aliwataja majeruhi waliokuwa kwenye  basi dogo ni  watoto wawili waliofiwa na mama yao katika   ajali hiyo ambao ni Catharine Mhagama (6) na Caltimei Mhangama  mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, Prisca Isaya (25), Chuki Wage (40), Anthon Cletus Mhando (39) mkazi wa eneo la SUA, Innocent Emilian , Willbrod Emilian ambao ni watu wazima mapacha , Iman Amri  Salum  na kondakta wa daladala hiyo  Ally Ramadhan.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi huyo  , chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi dogo ambaye ni marehemu kutaka kulipita lori la mchanga lililokuwa mbele  yake bila kuchukua tahadhari na hivyo kugonaga na basi la Kampuni ya New Force ambalo lilikuwa likiendeshwa na Mdula   Abdallah  (52) mkazi wa Dar es Salaam. Hata hivyo alisema , Polisi inamshirikia dereva  Mdula Abdallah wa Kampuni ya New Force kwa ajili ya uchunguzi zaidi  kutokana na ajali hiyo.
Alisema ,mazingira ya ajali hiyo inaonesha  huenda dereva wa basi hilo alikuwa katika mwendo kasi uliomsababishia ashindwe  kupunguza mwendo mara baada ya kuona  basi ndogo likilipita lori lililokuwa mbele ambapo ageweza   kunusuru ajali hiyo mbaya iliyopoteza maisha ya watu isitokee
 Askari Polisi wakishirikiana na wananchi wakiondoa mwili wa dereva wa basi dogo aina ya inayofanya safari zake Mlali- Moro Mjini baada ya kugongana na basi kubwa la New Force  namba T 346 DLY likitokea  Dar es Salaam – Tunduma ,  eneo la Lungemba – Rombo ,Manispaa ya Morogoro katika  barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
 Basi  la  New force New lenye namba T 346 DLY likitokea  Dar es Salaam kuelekea  Tunduma na kuhusika katika ajali hiyo.
 Baadhi ya wananchi wa maeneo ya mitaa ya kata zilizopo Manispaa ya Morogoro  wakiangalia ajali wa basi dogo Toyota Hiache inayofanya safari zake Mlali –  Moro mjini baada ya kugongana na basi kubwa la New Force  eneo la Lungemba – Rombo , katika  barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
 Mabaki  ya basi dogo Toyota Hiache inayofanya safari zake Mlali – Morogoro mjni kugongana na basi kubwa la New Force  eneo la Lungemba – Rombo , katika  barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
Wananchi wa kata za Manispaa ya Morogoro wakiliangalia basi kubwa la New Force namba T 346 DLY likitokea  Dar es Salaam – Tunduma  baada ya kugongana na basi dogo Toyota Hiache namba T 962 BSE inayofanya safari zake Mlali- Moro Mjini eneo la Lungemba – Rombo ,Manispaa ya Morogoro katika  barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro


Hivyo makala AJALI YA BASI NEW FORCE NA BASI DOGO TOYOTA HIACHE YASABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA KUJERUHI TISA KULAZWA WODINI HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO

yaani makala yote AJALI YA BASI NEW FORCE NA BASI DOGO TOYOTA HIACHE YASABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA KUJERUHI TISA KULAZWA WODINI HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AJALI YA BASI NEW FORCE NA BASI DOGO TOYOTA HIACHE YASABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA KUJERUHI TISA KULAZWA WODINI HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/ajali-ya-basi-new-force-na-basi-dogo.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "AJALI YA BASI NEW FORCE NA BASI DOGO TOYOTA HIACHE YASABABISHA VIFO VYA WATU WATANO NA KUJERUHI TISA KULAZWA WODINI HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO"

Post a Comment