SERIKALI YAICHAMBUA BAJETI YA MAZISHI YA AQWILINA

SERIKALI YAICHAMBUA BAJETI YA MAZISHI YA AQWILINA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAICHAMBUA BAJETI YA MAZISHI YA AQWILINA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAICHAMBUA BAJETI YA MAZISHI YA AQWILINA
kiungo : SERIKALI YAICHAMBUA BAJETI YA MAZISHI YA AQWILINA

soma pia


SERIKALI YAICHAMBUA BAJETI YA MAZISHI YA AQWILINA

*Baadhi ya matumizi hayatawezekana kwasababu za kisheria

Na Said Mwishehe,Globu wa Jamii

SERIKALI imesema imepokea bajeti ya gharama ya mazishi ya aliyekuwa Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha Usafirishaji (NIT) Aqwilina Akwiline(pichani enzi za uhai wake) ya Sh 80,150,000 kutoka kwa familia huku ikieleza baadhi ya matumizi hayatakubaliwa kwani kisheria hayagharamiwi na Serikali.

Pia imesema kwenye makisio hayo kuna gharama zilizokuwa zimepewa makadirio ya juu.Hivyo Serikali kupitia Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia jana jioni imekaa na familia ili kuondoa changamoto hiyo na hatimaye kupata bajeti ya pamoja.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mwasu Sware imesema Wizara hiyo kupitia kwa Katibu Mkuu wake  Dk.Leonard Akwilapo ilipokea makisio ya gharama za mazishi kiasi hayo kutoka kwa Msemaji wa familia hiyo Festo Kavishe. 

"Kumekuwepo na taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonesha makisio ya gharama za mazishi ya Aqwilina Akwiline. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaufahamisha umma kuwa bajeti hiyo inayosambaa kwenye mitandao ni makadirio yaliyoandaliwa na familia ya marehemu.

"Baada ya kupokea makisio hayo Katibu Mkuu Dk.Akwilapo alitahadharidha kuna baadhi ya matumizi hayatakubaliwa kwa kuwa kisheria hayagharamiwi na Serikali .Pia katika makisio hayo kuna gharama ambazo zilikuwa na makadirio ya juu,"amesema.

Amesema kutokana na hali hiyo Dk.Akwilapo aliagiza kuwe na kikao kati ya Wizara na ndugu wa marehemu ili kuweka sawa changamoto hizo ili kuwa na bajeti ya pamoja.Hivyo kikao kilifanyika jana jioni na kufikia muafaka."Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa taratibu nyingine za 
mazishi zinaendelea vizuri,"amesema Sware.



Hivyo makala SERIKALI YAICHAMBUA BAJETI YA MAZISHI YA AQWILINA

yaani makala yote SERIKALI YAICHAMBUA BAJETI YA MAZISHI YA AQWILINA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAICHAMBUA BAJETI YA MAZISHI YA AQWILINA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/serikali-yaichambua-bajeti-ya-mazishi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI YAICHAMBUA BAJETI YA MAZISHI YA AQWILINA"

Post a Comment