PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA.
kiungo : PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

soma pia


PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amewataka wakazi wa wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, kuilinda miundombinu ya barabara iliyokamilika kujengwa ili kupunguza gharama za matengenezo ambayo yanaepukika.
Ametoa rai hiyo Wilayani humo, baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na kusema kuwa barabara hiyo itawaunganisha wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa na kukuza uchumi kupitia mazao mbalimbali yanayolimwa kwenye mikoa hiyo.
"Barabara hii sasa imekamilika ni jukumu la kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie kuilinda na kuhakikisha inadumu kwa kipindi kilichokadiriwa", amesema Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa barabara hiyo itakuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi watakaotumia usafiri wa reli ya kisasa pindi utakapokamilika kwani watatoka kwenye mikoa ya jirani kupandia kwenye stesheni ya Malyampaka ambayo iko kwenye barabara hiyo.

Aidha, amewapongeza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo kwa usimamizi mzuri wa mradi huo na wananchi kwa kutoa ushirikiano kwa mkandarasi ili kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt. Seif Shekalaghe, ameishukuru Serikali kwa kukamilisha sehemu ya barabara hiyo na kumuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa miundombinu hiyo italindwa ili idumu muda mrefu.

"Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuikamilisha barabara hii kwa kiwango cha lami kwani kwa sasa muda na gharama za usafirishaji wa mazao zitapungua", amesema Dkt. Shekalaghe.

Naye Meneja wa TANROADS, mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent, amesema mradi mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 98 na kazi zilizobaki ni kuweka alama za barabarani na ujenzi umezingatia viwango vinavyohitajika.
Mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 imejengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya CHICO ambapo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 61.46 na zote zikiwa zimefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na  uongozi wa Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu, wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya miundombinu ya barabara mkoani humo. Wa Kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Seif Shekalaghe.
 Gari maalum likimwaga lami ya mwisho katika barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3, wilayani Maswa, Mkoani Simiyu. Ujenzi wa barabara hiyo umegharimu Serikali kiasi cha shilingi bilioni 61.46.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe kuhusu umuhimu wa kutunza barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, wilayani humo, mkoani Simiyu,
 Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3, wilayani humo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na Kushoto ni Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 kutoka kwa Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent (wa pili kulia), mara baada ya kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara hiyo, wilayani Maswa, mkoani Simiyu.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


Hivyo makala PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

yaani makala yote PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/prof-mbarawa-awataka-wananchi-wa-simiyu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "PROF. MBARAWA AWATAKA WANANCHI WA SIMIYU KUILINDA MIUNDOMBINU YA BARABARA."

Post a Comment