ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA

ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA
kiungo : ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA

soma pia


ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA

Na Joel Maduka,Geita.

Serikali Mkoani Geita Imeteketeza zana haramu zenye thamani ya shilingi milioni therathini na tatu zikiwemo Nyavu za makila zilizounganishwa 2,393,makokolo ya sangara 32,timba 142 makokoro ya dagaa 7 na dududu 11.

Hatua hiyo imetokana na oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea kwenye maeneo ya ziwa viktoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi huo ndani ya ziwa hilo pamoja na kuondoa mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Zoezi hili la uteketezaji zana hizo limefanyika kwenye Kata ya Nkome ,ambapo kiongozi wa oparesheni hiyo Gabriel Mageni ,amemweleza mkuu wa mkoa huo kwamba kuna baadhi ya wafanyakazi wa hifadhi ya Rubondo wamekuwa wakihusika na uvuvi haramu kwa kuwaruhusu wavuvi kuingia kwenye hifadhi na wengine kuficha zana zao ndani ya hifadhi na kwamba wamekuwa wakilipwa fedha wafanyakazi hao maarufu kwa jina la "KIFUNDA"

Kufuatia malalamiko hayo mtandao huu umetafuta kwa njia ya simu afisa mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete alisema kuwa wao kama watu ambao wanamamlaka ya hifadhi za taifa na kwamba kwa mujibu wa kanuni na taratibu za sheria askari wao hawapaswi kushiriki kwenye vitendo vya ujangili na kwamba taratibu za kiuchunguzi zikifanyika na wakabaini kuna watumishi wanajihusisha na vitendo hivyo hatua za kisheria na za kinidhamu zitachukuliwa na hawawezi kuwakingia kifua.

Aidha Mageni aliongeza kuwa katika operesheni hiyo ambayo ina siku kumi na mbili baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha serikali kukosa mapato.

Mkuu wa Mkoa huo,Mhandisi Robert Luhumbi,amewataadhalisha watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu na kwamba endapo kuna mtu hakibainika na kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua na kwamba kupitia oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo.

Nyawalwa Wange ni moja kati ya watu ambao wanajishughulisha na kazi ya uvuvi alisema agizo la Mkuu wa Mkoa ni la kuungwa mkono kutokana na kwamba uvuvi haramu umeendelea kuharibu kwa kiasi kikubwa samaki ambao wapo ndani ya ziwa viktoria na kwamba serikali iendelee kuwabaini wale wote ambao wanaendelea kufanya shughuli za uvuvi kinyume na sheria.

Katika oparesheni hiyo jumla ya fedha ambazo zimekusanywa ni zaidi ya milion, 111 fedha zinazotokana na faini ,malipo ya mrahaba pamoja na mauzo ya samaki.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita . 
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akielezea mikakati ya wilaya ya kuhakikisha wanapamba zaidi na vitendo ambavyo vimeendelea kufanywa na wavuvi ambao awana mapenzi mema na samaki waliomo kwenye ziwa viktoria wakati wa zoezi la uteketezaji wa zana haramu. 
Wananchi wa Kata ya Nkome wakiwa kwenye mkutano ambao ulikuwa na lengo la kuelezea hali ya uvuvi haramu ilivyo kwenye kata ya Nkome na namna ambavyo oparesheni imeweza kufanyika kwenye maeneo hayo. 
Kiongozi wa kikosi maalumu kinachoendesha oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu ziwa victoria Gabriel Mageni akielezea namna ambavyo wameweza kuendesha zoezi hilo ndani ya siku kumi na mbili. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisita kwa wale ambao ni watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu 


Hivyo makala ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA

yaani makala yote ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/zana-za-uvuvi-haramu-za-mamilioni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA"

Post a Comment