title : DKT.SHEIN AZINDUA SOKO LA KINYASINI
kiungo : DKT.SHEIN AZINDUA SOKO LA KINYASINI
DKT.SHEIN AZINDUA SOKO LA KINYASINI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Mohamed Shein amefungua Soko Jipya la Kinyasini lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) ili kutatua changamoto za kukosekana kwa soko la kisasa katika Mkoa wa Kaskazini litakalowasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo kuendesha biashara zao.
Mhe. Rais Shein amesema soko hilo litawagusa na kuwafikia watu wenye kipato cha chini kuinuka kiuchumi kwa kuwanufaisha Wajasiliamali wadogo wadogo vijijini pamoja na wafanyabiashara; Asasi ndogo ndogo za kifedha zinazotoa huduma vijijini; Vyama vya Msingi vya Ushirika/ Asasi za vijijini zinazojishughulisha na usindikaji wa mazao na masoko ya mazao kwa kushirikisha wanawake katika makundi yote.
Katika uzinduzi huo uliofanyika Januari 09, 2018 Mkoa wa Kaskazini katika eneo la Kinyasini, Mhe.Rais alisema kujengwa kwa soko hilo kuna manufaa makubwa kwa wakulima wadogo wakiwemo wafugaji, wavuvi na wafanya kazi za mikono.
“Soko hili litakuwa lenye tija kubwa kwa wananchi wa Zanzibar bila kujali maeneo wanakotoka. Soko hili ni letu sote, lisingeweza kujengwa kila mahali, au hewani lazima lingewekwa mahali, hivyo eneo hili la Kaskazini lilipata fursa hii, hivyo niwaombe liwe la wananchi wote wa Zanzibar.”Alisema Mhe.Rais
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Soko jipya la Kinyasini lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Januari 09, 2018 eneo la Kaskazin ‘A’ Zanzibar.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe.Jenista Mhagama na kushoto kwake ni Waziri wa Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
Mhandisi wa Kampuni ya ZECCON Bw.Ali Mbarouk Juma akitoa maelezo ya kitaalamu kuhusu ujenzi wa Soko la kinyasini kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wa uzinduzi wa Soko hilo lililojengwa eneo la Kaskazin ‘A’ Unguja, Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia Wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa Soko la Kinyasini lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akitoa maelezo mafupi ya Soko la Kinyasini wakati wa uzinduzi wa Soko hilo Januari 09, 2018 Lililojengwa katika mkoa wa Kaskazin ‘A’ Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akimpa mkono wa pongezi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama mara baada ya kuwasilisha maelezo mafupi kuhusu soko la Kinyasini lililozindulia Januari 09, 2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa Soko jipya la Kinyasini mara baada ya Uzinduzi Januari 09, 2018. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala DKT.SHEIN AZINDUA SOKO LA KINYASINI
yaani makala yote DKT.SHEIN AZINDUA SOKO LA KINYASINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT.SHEIN AZINDUA SOKO LA KINYASINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/dktshein-azindua-soko-la-kinyasini_10.html
0 Response to "DKT.SHEIN AZINDUA SOKO LA KINYASINI"
Post a Comment