title : NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA CHINA AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA.
kiungo : NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA CHINA AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA.
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA CHINA AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA.
Na Mary Gwera, Zanzibar
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim H. Juma ashauri juu ya uwezekano wa kuwa na Kanuni za pamoja za Sheria ya Biashara na Uwekezaji ‘Trade Investment Regulations’ kati ya Tanzania na China zitakazowezesha ukuaji wa uchumi ambao utasaidia kuleta maendeleo baina ya nchi hizi mbili.
Aliyasema hayo, Desemba 1, katika maongezi maalum na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wa China, Mhe. Zhao Dacheng, pindi alipotembelewa na Naibu Waziri huyo Mahakama Kuu-Zanzibar ambapo Mhe Jaji Mkuu anaendelea na Vikao maalum vya Mahakama ya Rufani ‘court session’
Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa; China ni nchi ambayo tayari imeshapiga hatua kubwa kiuchumi na kimaendeleo, hivyo kuwepo kwa Kanuni wezeshi za Biashara Uwekezaji baina ya nchi hizi mbili (2) utasaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania pia.
“Ni vyema kuangalia juu ya uwezekano wa nchi zetu; Tanzania na China kuwa na kanuni zinazofanana zitakazotoa muelekeo wa jinsi ya kuwekeza kwa manufaa ya pande zote mbili,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wa China, Mhe. Zhao Dacheng aliafiki ushauri huo uliotolewa na Mhe. Jaji Mkuu na kumtaka kuendelea na hatua za awali za uwasilishaji wa pendekezo hilo kwa taratibu zinazotakiwa kufanyika ili kufanikisha utekelezaji wa ushauri uliotolewa.
Mhe. Jaji Mkuu akifurahia zawadi ya picha aliyopatiwa na Mgeni wake.
Picha ya pamoja baada ya Majadiliano: wa nne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, katikati ni Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga pamoja na Wajumbe waliombatana na Naibu Waziri.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akimkaribisha Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng pindi alipowasili katika Ofisi ya Jaji Mkuu-Mahakama Kuu Zanzibar.
Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng (katikati) akiongea jambo na Mhe. Jaji Mkuu pindi alipomtembelea Desemba 01, 2017.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA CHINA AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA.
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA CHINA AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA CHINA AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/naibu-waziri-wa-katiba-na-sheria-wa_2.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA CHINA AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA."
Post a Comment