NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AZINDUA UMEME WA REA KATA YA MWASENI WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI

NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AZINDUA UMEME WA REA KATA YA MWASENI WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AZINDUA UMEME WA REA KATA YA MWASENI WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AZINDUA UMEME WA REA KATA YA MWASENI WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI
kiungo : NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AZINDUA UMEME WA REA KATA YA MWASENI WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI

soma pia


NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AZINDUA UMEME WA REA KATA YA MWASENI WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu amezindua mradi wa umeme wa vijijini REA awamu ya pili katika kijiji cha Mloka kata ya Mwaseni Rufiji  Mkoa wa Pwani sambamba na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Naibu Waziri aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo ambapo kwa pamoja waliweza kuzungumza na wananchi hao wakizidi kuwasisitiza kujiunganisha na mradi wa umeme wa REA kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi kwa nishati hiyo muhimu.

Kabla ya kuzinduliwa kwa umeme huo, Naibu Waziri wa Nishati Subira aliweza kupewa taarifa rasmi ya toka kuanza kwa mradi huo wa umeme vijijini REA kutoka kwa Meneja wa TANESCO kutoka Wilaya ya Rufiji Basilus Kayombo ambapo alisema kuwa mradi huo rasmi kwa kijiji cha Mloka ulianza mwaka 2014, na ujenzi wake kuanza 2015 na kumalizika Novemba 2017 na kugharimu takribani bilion 2.5 za kitanzania kutoka Ikwiriri mpaka kufika Mloka.

Akizungumza na wananchi baada ya kuzindua meadi wa umeme wa vijijini REA, Naibu Waziri wa Nishati ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira, alisema kuwa nia kubwa ya serikali kuleta huduma ya nishati karibu na wananchi ni katika kuchagiza maendeleo yakiwemo wananchi kwa pamoja kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kujiinua kiuchumi.

 Naibu Waziri Wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wakati wa ziara yake ya siku mbili ndani ya Wilaya ya Rufiji na kujionea maendeleo ya mradi wa umeme vijijini REA ulipofikia na kuwataka wananchi waendelee kujiunganisha kwa kujaza fomu ili kuweza kupata umeme kwa ajili ya kuchagiza maendeleo ya kiuchumi ndani ya mkoa wa Pwani.
 Meneja wa TANESCO Wilaya ya Rufiji, Sabilus Kayombo akielezea mradi wa umeme wa vijijini REA katika kata ya Mwasene wenye takribai Kilomita 100 kutoka Ikwiriri ulivyoanza mpaka kufikia tamati Novemba mwaka huu na kugharimu takribani bilioni 2.5 ulioanza kujengwa 2015.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akikagua baadhi Zahanati wakati wa ziara yake ya siku mbili ndani ya Wilaya ya Rufiji.
 Wananchi wa kijiji cha Kipo kata ya Kipugila wakionesha malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu ya kushindwa kupata umeme wa REA ingawa miundo mbinu ikiwemo nguzo za umeme zimepita katika maeneo yao Kijijini hapo na Naibu Waziri kuwaagiza TANESCO kuweza kuhakikisha kabla hawajaenda kata nyingine wahakikishe vijiji vyote vinne vinapata umeme huo.
Naibu Waziri Wa Nishati, Subira Mgalu akikagua kisima cha maji cha Kata ya Mkongo kinachoendesha kwa nguvu ya rasilimali ga mafuta kutokana na kutokuwa na nishati ya umeme kwenye eneo hilo na kupelekea wananhi kununua maji kwa bei kubwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AZINDUA UMEME WA REA KATA YA MWASENI WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI

yaani makala yote NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AZINDUA UMEME WA REA KATA YA MWASENI WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AZINDUA UMEME WA REA KATA YA MWASENI WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/naibu-waziri-nishati-subira-mgalu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AZINDUA UMEME WA REA KATA YA MWASENI WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI"

Post a Comment