KONGAMANO LA PETROLI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA KENYA 2019

KONGAMANO LA PETROLI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA KENYA 2019 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KONGAMANO LA PETROLI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA KENYA 2019, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KONGAMANO LA PETROLI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA KENYA 2019
kiungo : KONGAMANO LA PETROLI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA KENYA 2019

soma pia


KONGAMANO LA PETROLI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA KENYA 2019

Na Veronica Simba - Kampala
Kongamano na Maonesho ya Tisa ya masuala ya Petroli kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, yanatarajiwa kufanyika nchini Kenya, Machi 2019. Azimio hilo limepata baraka za Mkutano Ngazi ya Makatibu Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliofanyika Kampala, Desemba 1, mwaka huu.
Mkutano huo wa Makatibu Wakuu ni maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wenye lengo la kupitia nyaraka na taarifa za Maandalizi ya Mkutano wa Kazi wa Wakuu wa Nchi kabla ya kuziwasilisha kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliopangwa kufanyika mwezi Januari, 2018.
Kuteuliwa kwa Kenya kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo kubwa, kunatokana na mzunguko wa kawaida wa ratiba yake, ambapo makongamano yaliyotangulia yalifanyika katika nchi za Jumuiya husika kwa mlolongo wa Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi.
Hivyo basi, kutokana na mzunguko huo, Makatibu Wakuu wamebariki, Kongamano lijalo lifanyike Kenya kuanzia tarehe 6 hadi 8 Machi, 2019.
Aidha, Mkutano huo pia uliazimia kuwa, maandalizi ya Kongamano husika yaanze mapema ili kuwepo muda wa kutosha wa kujitangaza na kuvutia ushiriki wa mataifa mbalimbali duniani.
Masuala mengine yahusuyo nishati, yaliyojadiliwa katika Mkutano huo ni pamoja na maendeleo ya upembuzi yakinifu kwa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Kigali hadi Bujumbura, Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Mbarara – Mwanza - Isaka hadi Dar es Salaam, pamoja na kuoanisha mfumo wa kisheria na udhibiti wa masuala ya nishati.
Vilevile, Mkutano huo pia ulijadili maendeleo endelevu ya Kituo cha Ubora (Centre of Excellence) cha masuala ya Nishati Jadidifu na Matumizi Bora ya Nishati katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichopo kwenye Kitivo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Makerere, nchini Uganda.
Mbali na masuala ya nishati, sekta nyingine zilizojadiliwa katika Mkutano huo ni elimu ya juu, miundombinu, uchukuzi, fedha pamoja na afya.
Tanzania, kama ilivyokuwa kwa nchi nyingine wanachama, iliwakilishwa na wataalam mbalimbali kutoka sekta husika pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo akiwamo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto), akishiriki katika Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala hivi karibuni. Pamoja naye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati) na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson Mdemu.
 Mwakilishi kutoka Tanzania, ambaye ni Ofisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Steven Mbundi (kushoto), akisaini makubaliano ya masuala mbalimbali yaliyojadiliwa katika Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu Kampala, sambamba na wenzake kutoka nchi nyingine za Jumuiya hiyo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto), akijadiliana jambo na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Petroli, James Andilile (katikati) na Mhandisi Nishati, Samuel Mgweno, muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu.
 Sehemu ya Ujumbe wa Wataalam kutoka Tanzania, wakiwa katika Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliofanyika Kampala, Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu.
 Meza Kuu – Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala, Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu.

Wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala, Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu, wakiendelea na Mkutano.


Hivyo makala KONGAMANO LA PETROLI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA KENYA 2019

yaani makala yote KONGAMANO LA PETROLI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA KENYA 2019 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KONGAMANO LA PETROLI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA KENYA 2019 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/kongamano-la-petroli-afrika-mashariki.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KONGAMANO LA PETROLI AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA KENYA 2019"

Post a Comment