title : WANAFUNZI SHULE YA MUGABE MANISPAA YA UBUNGO HATARINI KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU.
kiungo : WANAFUNZI SHULE YA MUGABE MANISPAA YA UBUNGO HATARINI KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU.
WANAFUNZI SHULE YA MUGABE MANISPAA YA UBUNGO HATARINI KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU.
MwambawahabariNa .John Luhende
Kamati ya kudhibiti UKIMWI halmashauri ya Manispaa ya ubungo imebaini kuwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mugabe wanajihusisha vitendo vya ushoga na biashara ya ngono na kusababisha kuenea kwa maambukizi mapya VVU.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo,Ramadhani Kwangaya wakati akitoa taarifa hiyo kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa ya ubungo lililo Keti kwaajili ya kupokea taarifa ya miradi ya maendeleo ya robo ya kwanza , utendaji , uwajibikaji wa idara mbalimbali na taarifa za kamati za halmashauri hiyo.
" Shule hiyo iko kwenye mazingira hatarishi ambapo baadhi ya wanafunzi wamejiingiza kwenye mambo ya ushoga na biashara ya ngono hivyo inatakiwa ichukuliwe hatua haraka sana,"alisema Kwangaya.
Diwani wa kata ya Kibamba,Mgawe Stanley ameiomba kamati hiyo kwenda eneo maarufu linaloitwa kwa Neema ili kuwasaidia wananchi wanaokaa karibu na vilabu vya pombe za kienyeji ili wapewe elimu kwa kuwa maambukizi yapo juu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John Kayombo amesema mwaka huu wa fedha wa 2017/18 manispaa hiyo ilitenga kiasi cha fedha sh 1 bilioni ambazo zimetokana na mapato ya ndani ya halmashauri hiyo ambayo itatumika kwa ajili kulipa madeni na kuboresha utendaji wa Manispaa hiyo .
Naye Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob amewataka Madiwani wa Manispaa hiyo kuwaelimisha wananchi na wamiliki wa shule ambazo hazijasajiliwa kuwa kufanya usajili ili kuepusha usumbufu wa kufungiwa na
Jacob alisema baada ya Madiwani kuhoji kuhusu Manispaa hiyo kuzifunga shule zote zisizo na usajili na kuibua maswali mengi kuhusu uhalali wa zoezi hilo, ambapo amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuzifugia shule hadi watakapo jisajili.
Katika hatua nyingine Madiwani, wameitaka TARURA na TANROAD, kukarabati barabara na madaja yaliyo haribika na mvua ili yaweze kupitia na kusaidia wananchi katika shughuli zao za kiuchumi.
Hivyo makala WANAFUNZI SHULE YA MUGABE MANISPAA YA UBUNGO HATARINI KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU.
yaani makala yote WANAFUNZI SHULE YA MUGABE MANISPAA YA UBUNGO HATARINI KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI SHULE YA MUGABE MANISPAA YA UBUNGO HATARINI KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/wanafunzi-shule-ya-mugabe-manispaa-ya.html
0 Response to "WANAFUNZI SHULE YA MUGABE MANISPAA YA UBUNGO HATARINI KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU."
Post a Comment