title : SERIKALI YAREJESHA UMILIKI HALALI WA KIWANJA KILICHOUZWA KWA HATI ZA KUGHUSHI
kiungo : SERIKALI YAREJESHA UMILIKI HALALI WA KIWANJA KILICHOUZWA KWA HATI ZA KUGHUSHI
SERIKALI YAREJESHA UMILIKI HALALI WA KIWANJA KILICHOUZWA KWA HATI ZA KUGHUSHI
Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma
Serikali imerejesha hati ya Kiwanja Namba 9331 kilichopo kitalu namba 91 Msalato Dodoma kwa mmiliki wake halisi Bw. Sagaf Omari na Bi Madina Hassan ambao ni wamiliki halali wa kiwanja hicho kilichouzwa kwa Bw. Lucas Mlay wa Jijini Dar es Salaam kwa shilingi milioni 35 kwa njia zisizo halali.
Akizungumza wakati akimkabidhi hati hiyo Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kuwa kiwanja hicho chenye ukubwa wa takribani hekta mbili na nusu kiliuzwa bila mmiliki halali wa kiwanja hicho kuwa na taarifa kupitia kwa wanasheria wasio waaminifu waliosaidia kutaka kufanikisha wizi wa kiwanja hicho.
“Niwatahadharishe Mawakili wote na wanasheria ambao wanashirikiana na watu wasio waaminifu kutaka kudhulumu viwanja vya wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itawachukuliwa hatua kali za kisheria na kwa kuanza tutaanza na hawa mawakili waliofanikisha mchezo huu wakumdhulumu mama huyu na mume wake kiwanja chao wanachomiliki kihalali” Alisisitiza Lukuvi
Akifafanua Waziri Lukuvi amesema kuwa Wizara yake imejiridhisha kuwa nyaraka zilizowasilishwa ili kubadilisha umiliki wa kiwanja hicho ni za kughushi na wamiliki halali wa kiwanja hawakuwa na taarifa kuhusu kuuzwa kwa kiwanja chao hadi walipopata taarifa kwa majirani na kuamua kuchukua hatua kwa kuwasilisha malalamiko yao katika Ofisi yake.
Hivyo makala SERIKALI YAREJESHA UMILIKI HALALI WA KIWANJA KILICHOUZWA KWA HATI ZA KUGHUSHI
yaani makala yote SERIKALI YAREJESHA UMILIKI HALALI WA KIWANJA KILICHOUZWA KWA HATI ZA KUGHUSHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAREJESHA UMILIKI HALALI WA KIWANJA KILICHOUZWA KWA HATI ZA KUGHUSHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/serikali-yarejesha-umiliki-halali-wa.html
0 Response to "SERIKALI YAREJESHA UMILIKI HALALI WA KIWANJA KILICHOUZWA KWA HATI ZA KUGHUSHI"
Post a Comment