title : Mwanafunzi wa chuo Kikuu ajiua Baada ya Kufeli
kiungo : Mwanafunzi wa chuo Kikuu ajiua Baada ya Kufeli
Mwanafunzi wa chuo Kikuu ajiua Baada ya Kufeli
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udaktari cha Imtu, Daniel Mabisi miaka 28 anadaiwa kujinyonga hadi kufa baada ya kufeli mitihani mara mbili mfululizo.
Taarifa zilizopatikana zinadai siku mbili kabla ya kujinyonga, mwanachuo huyo alionekana mtaani kwao Mgeninani, Kata ya Kijichi jijini Dar es salaam ambako jana alijinyonga majira ya saa saba mchana baada ya kutoka chuo alikokuwa akisoma.
Akizungumza kwa simu kutoka Morogoro, baba mdogo wa marehemu, Joseph Lukuba alisema kuwa “Nimepigiwa simu mchana huu nikaambiwa Daniel amejinyonga, nimeshtuka kwa sababu ni juzi tu tulimtumia nauli ili arudi nyumbani Mwanza baada ya kupata taarifa kuwa amefeli kwa mara nyingine,” alisema Lukuba.
Alisema uamuzi aliouchukua unasikitisha kwa kuwa kufeli, isingekuwa sababu ya kushindwa maisha hadi kufikia uamuzi wa kujinyonga.
“Kama familia tumehama na tuko mbali kikazi, tumemuomba jirani asimamie suala hili wakati taratibu za mazishi au kusafirisha mwili zikiendelea,” alisema Lukuba.
Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa Mtaa wa Mgeninani, Khuruka Mwinyimvua alisema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kukuta mwili ukiwa umening’inia juu ya mwembe.
“Kijana huyo alionekana tangu juzi akizunguka mtaani hapa baada kurejea kutoka chuoni anakosoma, alionekana kama mtu asiyekuwa na furaha,” alisema Mwinyimvua na kuongeza: “Hadi sasa mwili umechukuliwa na polisi kwa taratibu nyingine.”
Naye kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula alithibitisha kupokea taarifa za kujinyonga kwa kijana huyo na kuwaagiza askari walio karibu na maeneo hayo kuchukua mwili huo.
Hivyo makala Mwanafunzi wa chuo Kikuu ajiua Baada ya Kufeli
yaani makala yote Mwanafunzi wa chuo Kikuu ajiua Baada ya Kufeli Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mwanafunzi wa chuo Kikuu ajiua Baada ya Kufeli mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/mwanafunzi-wa-chuo-kikuu-ajiua-baada-ya.html
0 Response to "Mwanafunzi wa chuo Kikuu ajiua Baada ya Kufeli"
Post a Comment