Katekista Afariki baada ya kumaliza Ibaada ya Mazishi

Katekista Afariki baada ya kumaliza Ibaada ya Mazishi - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Katekista Afariki baada ya kumaliza Ibaada ya Mazishi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Katekista Afariki baada ya kumaliza Ibaada ya Mazishi
kiungo : Katekista Afariki baada ya kumaliza Ibaada ya Mazishi

soma pia


Katekista Afariki baada ya kumaliza Ibaada ya Mazishi

Mwalimu wa dini wa Kanisa Katoliki (katekista) Jimbo la Mpanda,mkoani Katavi Noel Sitemele amefariki dunia muda mfupi baada ya kumaliza kuongoza ibada ya mazishi ya muumini wake yaliyofanyika katika makaburi ya Mchakamchaka Kijiji cha Majalila wilayani Tanganyika mkoani Katavi.

Katekista huyo alikuwa akitoa huduma ya kiroho katika Kigango cha Mchakamchaka kilichopo katika Parokia ya Mpanda Ndogo katika Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi. 

Akizungumzia mkasa huyo, Diwani wa Kata ya Mpanda Ndogo, Hamad Mapengo alisema licha ya Sitemele kuwa mwalimu wa dini, katika uhai wake alikuwa pia Mwenyekiti wa Kijiji cha Majalila kilichopo katika Halmashauri ya Mpanda wilayani Tanganyika.

Mapengo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda, alisema Katekista alifariki dunia juzi saa 11 jioni muda mfupi baada ya kufikishwa zahanati ya kijiji Majalila kutibiwa.

Alisema kabla ya kukutwa na umauti, Katekista huyo alikuwa mwenye siha njema na aliongoza ibada ya mazishi ya muumini wake hadi mwisho katika makaburi ya Kigango cha Mchakamchaka kilichopo katika Kijiji cha Majalila ambapo alianza kujisikia vibaya.

“Baada ya kumaliza ibada hiyo ya mazishi, alianza kujisikia vibaya hivyo akalazimika kurejea nyumbani kwake na kuwaacha waombolezaji makaburini,” alieleza Mpaengo.

 Alisema, baada kufika nyumbani kwake, hali yake iliendelea kuwa mbaya na aliomba msaada kutoka kwa majirani zake wamkimbize kwenye kituo cha afya kwa matibabu.

Inaelezwa zahanati hiyo haiko mbali kutoka alikokuwa akiishi mwalimu huyo wa dini. 

Mwenyekiti alisema, taarifa za kifo cha Katekista huyo zilizagaa haraka kijijini humo na kuwafikia waombolezaji waliokuwa nyumbani kwa marehemu aliyeongozewa ibada ya mazishi na Katekista huyo waliopata simanzi kubwa wengine wakiwa hawaamini jambo hilo.

Maziko yake yalifanyika jana makaburi ya kigango cha Mchakamchaka Kijiji cha Majalila. Padri Paschal Kipenye wa Parokia ya Mpanda Ndogo aliongoza ibada ya mazishi yaliyohudhuriwa na mamia ya waombolezaji akiwemo Mbunge wa Mpanda Vijijini, Selemani Kakoso.

IMEANDIKWA NA PETI SIYAME - HABARILEO


Hivyo makala Katekista Afariki baada ya kumaliza Ibaada ya Mazishi

yaani makala yote Katekista Afariki baada ya kumaliza Ibaada ya Mazishi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Katekista Afariki baada ya kumaliza Ibaada ya Mazishi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/katekista-afariki-baada-ya-kumaliza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Katekista Afariki baada ya kumaliza Ibaada ya Mazishi"

Post a Comment