KATIBU MKUU PROF. ELISANTE OLE GABRIEL ATEMBELEA KIWANDA CHA HUANRI MEDICAL GROUP BEIJING NCHINI CHINA

KATIBU MKUU PROF. ELISANTE OLE GABRIEL ATEMBELEA KIWANDA CHA HUANRI MEDICAL GROUP BEIJING NCHINI CHINA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KATIBU MKUU PROF. ELISANTE OLE GABRIEL ATEMBELEA KIWANDA CHA HUANRI MEDICAL GROUP BEIJING NCHINI CHINA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KATIBU MKUU PROF. ELISANTE OLE GABRIEL ATEMBELEA KIWANDA CHA HUANRI MEDICAL GROUP BEIJING NCHINI CHINA
kiungo : KATIBU MKUU PROF. ELISANTE OLE GABRIEL ATEMBELEA KIWANDA CHA HUANRI MEDICAL GROUP BEIJING NCHINI CHINA

soma pia


KATIBU MKUU PROF. ELISANTE OLE GABRIEL ATEMBELEA KIWANDA CHA HUANRI MEDICAL GROUP BEIJING NCHINI CHINA

Mwambawahabari

Katibu
mkuu wa  Wizara ya Viwanda ya Biashara na Uwekezaji,  Prof  Elisante 
 Ole Gabriel  akiwa katika ziara ya kikazi nchini China  (Beijing)
ametembelea kiwanda cha  Huanri Medical Group kinachojishughilisha na
utengenezaji wa vifaa tiba, Mitungi ya Gesi na Matairi.

Akiwa
kiwandani hapo alishuhudia baadhi ya  Vifaa vya tiba vinavyongenezwa
kiwandani  hapo Fingertip/Handheld Oximeter ambacho hutumika kupima
kiwango cha hewa ya Oxygen katika damu  (vinawafaa zaidi  wakina mama
waja wazito na wazee), Anesthesia Machine inayotumika katika upasuaji
mkubwa  pale ambapo mtu amewekewa dawa ya usingizi, Ventilator
inayotumika ICU kwa ajili ya kusaidia upumuaji kwa mgonjwa aliyezidiwa
pamoja na Kifaa kinachofahamika kama Health Machine (Mfano wa Briefcase)
kilichotengenezwa mahususi kwa ajili ya soko la  bara la Afrika na
kinaweza kutibu takribani magonjwa  16  na kinabeba vifaa vingi ndani
yake.

 Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwezeshaji Prof. Elisante Ole
Gabriel akishiriki katika kuunganisha Mashine inayofahamika kama 
"Anesthesia Machine" inayotumika katika usaidizi wa shughuli za 
Upasuaji Mkubwa.

 Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Prof. Elisante Ole
Gabriel (Katikati) pamoja na ujumbe alioambatana nao, alipotembelea
kiwanda cha Huanri Medical Group jijini Beijing nchini China.

 Akieleza
lengo la kutembelea kiwanda hicho  Prof. Elisante alisema ni 
kuzibaini  fursa za uwekezaji zilizopo na jukumu la wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji ni kuhakikisha kwamba wanajenga mazingira ya  ya
wawekezaji  kuwekeza vizuri bila kupoteza muelekeo  na lengo kubwa la
kuinua Uchumi wetu. “tungependa tuwe na mikataba ambayo kwa vyovyote
vile  hata kizazi kijacho kikija kuangalia hayo makubaliano  kifurahi na
kuthamini kwamba  waliongia katika makubaliano waliona mbele na
walijali maslahi mapana ya  taifa.

Tunachoamini 
ni kwamba wenzetu hawa wachina  katika tasnia mbalimbali watakuja
Tanzania watawekeza,  jukumu letu kubwa sisi  na tunachokifanya ni
kuendelea kuwavutia kuwaweka katika mlengo ambao watafanya kazi zao
vizuri  katika mazingira wezeshi na rafiki ili mwisho wa siku  ajira
ziongezeke  katika nchi yetu ya Tanzania  lakini pia tuweze kuuza vifaa 
vingi sana kutoka Tanzania kwenda kwenye masoko ya nje  kwa ajili ya
kupata fedha za kigeni  lakini lingine ambalo ni siri kubwa ya
mafanikio  ni kupata pia utaalam  ili vijana wa kitanzania waweze kupata
taaluma hii  ambayo ni ya kiwango cha  juu”  Alisema Prof. Elisante.

  akifanya mahojiano na vyombo vya habari baada ya kuhitimisha ziara yake kiwandani hapo 

 Akitazama moja ya hatua za kutengenezaji wa Vifaa vya Tiba kiwandani hapo

 Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole
Gabriel akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Huanri Medical Group Bw. Wang
qianjun Mara baada ya kuwasili kiwandani hapo.

 Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.Elisante Ole
Gabriel akizungumza jambo na Viongozi kutoka China - Asia Economic 
Development Association Overseas Cooperation Committee, alioambatana nao
Kiwandani hapo.

 
Akionyesha furaha yake  Katibu Mkuu  alisema tayari Huanri Medical
Group wamekubali walau kwenye masuala ya  taaluma ya vifaa tiba 
wataweza kuwaalika vijana wetu wa kitanzania waje wakae China kwa
takribani miezi mitatu ili wapate utaalam wa kuunganisha vifaa hivi vya
tiba  lakini lengo la serikali yetu ni kuona  kiwanda hiki kikijengwe
Tanzania  na hatua hii itapanua wigo wa ajira na pato la taifa litazidi
kuongezeka.

Huanri Medical Group  ni miongoni  mwa kundi kubwa la wawekezaji 
wanaotarajia kuja  Tanzania Mwezi Machi 2018 kwa ajili  ya mikutano
mbalimbali ya uwekezaji  na sisi tunawahakikishia kwamba serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Rais  Dr. John Pombe Magufuli 
inawakaribisha sana, na imani yetu ni kwamba Changamoto ya ajira itaweza
kupungua pale tutakapoendelea kuleta wawekezaji nchini.” Alisema  Prof
Elisante.

Akihitimisha
ziara hiyo katika kiwanda hicho  Prof. Elisante amewataka watanzania
kuendelea kupenda vitu vinavyozalishwa katika Taifa letu  na kununua
vitu vyetu vya ndani. Amesema  jambo la muhimu na kubwa ni  upatikanaji
wa uhamisho wa technolojia kutoka China  na kwamba tayari  Tanzania
imeahidi kufanya kazi na wawekezaji  hao  kwa  ushirikiano  kwa lengo
la  kuhakikisha ndoto na falsafa hii ya serikali ya awamu ya tano 
inakamilika na kufikiwa kwa  kwa kasi nzuri.”

Kwa
upande wake Rais wa kampuni hiyo ya Huanri Medical Group Bw. Wang
qianjun amefurahishwa na juhudi ambazo zinafanywa na Serikali ya
Tanzania kwenye sekta ya viwanda  na ameahidi ushirikiano mkubwa na 
kuonyesha utayari wake wa kuwekeza Tanzania .

Katika
ziara hiyo Katiba Mkuu  wa Wizara ya  Viwanda,Biashara na Uwekezaji
Prof. Elisante Ole Gabriel aliambatana na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa
Tanzania nchini China Said Massoro, Viongozi kutoka  China - Asia
Economic Development  Association Overseas Cooperation  Committee (Naibu
Katibu Mkuu Bi.  Rui LU na Makamu wa Rais Bi. Tian Wenhui) Bw.Remidius
Emmanuel  Katibu Mkuu wa  Shirikisho la Wanafunzi Watanzania nchini
China pamoja  Bi. Muka Kamuzora  Mtanzania anayesoma  Masuala ya Uchumi
hapa China.


Hivyo makala KATIBU MKUU PROF. ELISANTE OLE GABRIEL ATEMBELEA KIWANDA CHA HUANRI MEDICAL GROUP BEIJING NCHINI CHINA

yaani makala yote KATIBU MKUU PROF. ELISANTE OLE GABRIEL ATEMBELEA KIWANDA CHA HUANRI MEDICAL GROUP BEIJING NCHINI CHINA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU PROF. ELISANTE OLE GABRIEL ATEMBELEA KIWANDA CHA HUANRI MEDICAL GROUP BEIJING NCHINI CHINA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/katibu-mkuu-prof-elisante-ole-gabriel_28.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KATIBU MKUU PROF. ELISANTE OLE GABRIEL ATEMBELEA KIWANDA CHA HUANRI MEDICAL GROUP BEIJING NCHINI CHINA"

Post a Comment