title : BENKI YA KILIMO YATEMBELEA ENEO LA MRADI LA UMWAGILIAJI LA MWAMANYILI WILAYANI BUSEGA
kiungo : BENKI YA KILIMO YATEMBELEA ENEO LA MRADI LA UMWAGILIAJI LA MWAMANYILI WILAYANI BUSEGA
BENKI YA KILIMO YATEMBELEA ENEO LA MRADI LA UMWAGILIAJI LA MWAMANYILI WILAYANI BUSEGA
Katika kutekeleza kwa vitendo maagizo ya serikali ya kuchochea mapinduzi ya kilimo, Bodi ya wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetembelea eneo utakaofanyika mradi wa kilimo cha kisasa cha umwagiliaji la Mwamanyili Wilayani Busega mkoani Simiyu.
Akizungumza lengo la ziara hiyo, mkuu wa msafara huo ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila amesema lengo kubwa la kuanzishwa kwa Benki ya Kilimo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwakwamua wakulima nchini kutoka katika kilimo cha kujikimu na kwenda kwenye kilimo cha kibiashara ili waweze kujiongezea kipato.
Aliongeza kuwa Mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji ukianza kufanya kazi utatimiza malengo hayo ya Benki kwani utasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuwainua wananchi Kiuchumi na kukabiliana na upungufu wa chakula wakulima watakaolima katika skimu hiyo.
“Benki ya Kilimo ipo tayari kuunga mkono miradi ya aina hii ambayo inalenga katika kuendeleza miundombinu muhimu ikiwemo ya uendelezaji wa skimu za umwagiliaji, usafirishaji, hifadhi ya mazao, usindikaji, pamoja na masoko ili kumuongezea mkulima kipato,” alisema.
Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Eng. Tumbu akitoa maelekezo kwa ugeni kutoka TADB juu ya chanzo cha maji cha maji kitakachotumika katika mradi wa umwagiliaji wa Mwamanyili.
Muonekano wa eneo likalotumika kwa ajili ya mradi wa kilimo umwagiliaji wa Mwamanyili.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (aliyenyanyua mikono) akihimiza jambo wakati walipotembelea eneo likalotumika kwa ajili ya mradi wa kilimo umwagiliaji wa Mwamanyili.
Hivyo makala BENKI YA KILIMO YATEMBELEA ENEO LA MRADI LA UMWAGILIAJI LA MWAMANYILI WILAYANI BUSEGA
yaani makala yote BENKI YA KILIMO YATEMBELEA ENEO LA MRADI LA UMWAGILIAJI LA MWAMANYILI WILAYANI BUSEGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA KILIMO YATEMBELEA ENEO LA MRADI LA UMWAGILIAJI LA MWAMANYILI WILAYANI BUSEGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/benki-ya-kilimo-yatembelea-eneo-la.html
0 Response to "BENKI YA KILIMO YATEMBELEA ENEO LA MRADI LA UMWAGILIAJI LA MWAMANYILI WILAYANI BUSEGA"
Post a Comment