title : ANSAF YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA MAAFISA UGANI KWENYE HALMASHAURI
kiungo : ANSAF YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA MAAFISA UGANI KWENYE HALMASHAURI
ANSAF YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA MAAFISA UGANI KWENYE HALMASHAURI
NA KAROLI VINSENT
SERIKALI imeshauriwa kuwaongeza Maafisa Ugani kwenye halmashauri mbalimbali nchini ili waweza kumsaidia Mkulima aweze kufanya Kilimo kwa Ufanisi .
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Jukwaa la wadau wa Kilimo (ANSAF), Audax Rukongwe wakati wa mkutano uliowashirikisha wadau mbalimbali wa Kilimo kujadili kuhusu huduma za Ugani kwa kulima ili ziendane na shughuli ya Viwanda hapa nchini.
Amesema kitendo cha sasa cha kumtumia Afisa Mgani mmoja katika Kijiji kimoja ni kitendo ambacho hakiwezekani katika kumsaidia Mkulima.
“Afisa Ugani katika Kijini Kimoja, ni kitu hakiwezekani,maana leo tunasema tuna kijiji kimoja na kesho tukawa na vijiji ishirini hivyo itashindikana kwa afisa Ugani huyu kufanya kazi kwenye vijiji vyote, ni vema serikali ikaliangalia hili”Amesema Rukongwe.
Amesema kutokana na hali ilivyo ya uchache wa Maafisa Ugani kunahaja ya sekta binafsi kuwekeza kwenye utoaji wa Huduma ya Ugani kwa Wakulima ili iwe rahisi kwa Mkulima kusaidika.
“Sasa kuna haja sekta binafsi kuwekeza kwenye kutoa huduma ya Ugani kwa wakulima ili waweze kulipia kwa kiasi husika cha fedha, kwa mfano kwa wale wakulima wafugaji kama Ngome anaumwa Nyumbani hanahaja ya kumsubili aje Afisa Ugani bali anamtafuta Afisa ugani wa Sekta Binafsi anampa hela anamsadia “Amesema Rukongwe.
Kwa Upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokine (SUA)Dk Sizya Lugeye ambaye ni miongoni wa wadau hao katika mkutano huo, ameishauri serikali kuhakikisha wanawaongezea nguvu za maafisa Ugani waliopo ikiwemo kuwapata fedha pamoja vitendea kazi ili waweze kufanya kazi kwa ufanizi zaidi katika kuwahudumia wakulima.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la wadau wa Kilimo, Audax Rukongwe akizungumza na Waandishi wa habari leo wakati wa Mkutano wa wadau wa Kilimo ili kujadilia masuala mbalimbali yanahusu Kilimo.
Hivyo makala ANSAF YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA MAAFISA UGANI KWENYE HALMASHAURI
yaani makala yote ANSAF YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA MAAFISA UGANI KWENYE HALMASHAURI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ANSAF YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA MAAFISA UGANI KWENYE HALMASHAURI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/ansaf-yaishauri-serikali-kuongeza.html
0 Response to "ANSAF YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA MAAFISA UGANI KWENYE HALMASHAURI"
Post a Comment