title : MAJERUHI WAONGEZEKA SIMBA, SASA NI BOCCO NA MBONDE
kiungo : MAJERUHI WAONGEZEKA SIMBA, SASA NI BOCCO NA MBONDE
MAJERUHI WAONGEZEKA SIMBA, SASA NI BOCCO NA MBONDE
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KIKOSI cha Simba kimeanza kuandamwa na majeruhi baada ya John Bocco na Salim Mbonde kuungana na wachezaji wengine baada ya kuumia katika
mchezo wa ligi kuu Tanzania bara Jumapili iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar na kushindwa kuendelea mchezo baada ya kupata majeraha.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba Hajji Manara amesema kuwa kwa sasa wachezaji wote wapo katika uangalizi wa daktari wa timu.
Amesema beki wa kati Salim Mbonde ambaye ni tegemeo katika safu ya ulinzi ya Simba atakuwa nje kwa wiki nne baada ya kuumia goti katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa mwishoni mwa wiki iliyopita na atakosa michezo takribani minne ikiwemo Njombe Mji, Yanga, lakini pia anaweza akakosa mechi nyingine mbili dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City.
Ripoti ya madaktari inasema maumivu yake sio makubwa sana lakini anahitaji kukaa nje kwa ajili ya kutumia dawa lakini kama itakuwa vinginevyo basi tutawataarifu.
Hivyo makala MAJERUHI WAONGEZEKA SIMBA, SASA NI BOCCO NA MBONDE
yaani makala yote MAJERUHI WAONGEZEKA SIMBA, SASA NI BOCCO NA MBONDE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAJERUHI WAONGEZEKA SIMBA, SASA NI BOCCO NA MBONDE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/majeruhi-waongezeka-simba-sasa-ni-bocco.html
0 Response to "MAJERUHI WAONGEZEKA SIMBA, SASA NI BOCCO NA MBONDE"
Post a Comment