Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola

Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola
kiungo : Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola

soma pia


Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola

Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC, leo wametangaza uzinduzi wa kampeni ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa.

Nishati inayotumia nguvu ya jua (Sola) na bidhaa za taa zimekuwa zikihitajika zaidi nchini Tanzania, Nchi ambayo familia nyingi za vijijini zinategemea taa za sola zilizo katika viwango duni na bidhaa zingine za umeme kwaajili ya mwanga. Taa ambazo zinaharibika kwa haraka sana na kuwasababishia wateja na watumiaji kupoteza gharama kubwa, jambo ambalo linapunguza uaminifu wao katika uhalali wa bidhaa za sola. 

Kampeni hiyo, iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” ina lengo la kuongeza ufahamu wa watumiaji kuhusu manufaa ya taa za kisasa za sola zenye ubora, ambazo zinasaidia wanajamii kufanya maamuzi yenye uhakika wakati wa manunuzi. Itakuwa inaonyesha aina mbalimbali za taa za sola ambazo zina waranti ambazo zinakidhi viwango vya mwanga ulimwenguni (Lighting Global Quality Standard) kampeni hii vile vile inatoa mbinu za kibunifu za biashara katika nishati ya sola kama vile huduma ya Pay-As-You-Go (PAYGO), huduma ya malipo kwa njia ya simu ambayo inamuwezesha mnunuzi kulipa kidogo kidogo, ambayo inafanya makundi mbalimbali yenye uwezo mdogo kifedha kumudu gharama za bidhaa hizo. 

“Kampeni ya Lighting Africa inataka kuongeza kasi ya matumizi ya bidhaa zenye kiwango bora na zenye gharama nafuu, na inaweza kuboresha kiwango cha maisha ya wanajamii wa vijijini, ambao mara nyingi hutumia bidhaa za mafuta ya taa ambazo sio za uhakika na zina gharama kubwa kama vyanzo vyao vya mwanga.
Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Edward Ishengoma, akiashiria uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” na kampuni ya Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Prof. Egid Mubofu na kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa IFC-Banki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Uganda na Sudan Kusini, Dan Kasirye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga(K) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi.
Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Edward Ishengoma (Kushoto), akipata maelezo kuhusu bidhaa za sola kutoka kwa Meneja Mkazi wa Kampuni ya Solar Sister, Fatma Muzo,(katikati), pembeni yake ni ANSILA MAKUPA- BUSINESS DEVELOPMENT ASSOCIATE wakati wa uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” na kampuni ya Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam mapema iliyopita.
wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo mapema wiki iliyopita.




Hivyo makala Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola

yaani makala yote Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/lighting-africatanzania-imezindua.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola"

Post a Comment