Nchi sita kushiriki mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika

Nchi sita kushiriki mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Nchi sita kushiriki mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Nchi sita kushiriki mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika
kiungo : Nchi sita kushiriki mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika

soma pia


Nchi sita kushiriki mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika

Rwanda na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.

Nchi hizo mbili zinaungana na nchi nyingine sita zilizothibitisha kufanya hivyo awali kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Chama Cha kuogelea nchini (TSA), Leena Kapadia.
Kapadia amezitaja nchi hizo kuwa ni Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Uganda, Djibouti na wenyeji Tanzania. Kapadia amesema kuwa bado wametoa nafasi kwa nchi nyingine kuthibitisha kushiriki hadi wiki moja kabla ya mashindano ili kuleta mvuto na ushindani zaidi.

“Tumezipa nafasi zaidi kutafuta fedha ili kushiriki, tutafunga mlango wa kuthibitisha wiki moja kabla ya mashindano,” alisema Kapadia.

Alisema kuwa TSA bado inatafuta wadhamini kwa ajili ya kufanisha mashindano hayo na mpaka sasa kampuni za simu ya Vodacom Tanzania imethibitisha kudhamini mashindao hayo kama wadhamini wakuu.
Kampuni hiyo itagharimia medali na vikombe. Wadhamini wengine ni JCDecaux (billboards), Label Promotions (billboards), Print Galore na Slipway Hotel.

Pia kampuni ya ndege ya Swissair imejithibitisha kudhamini tiketi za ndege za waogeleaji wa Tanzania ambao wanasoma nchini Uingereza ambao wapo kwenye timu ya Taifa. Waogeleaji hao ni Sonia Tumiotto, Smriti Gokarn, Anjani Taylor, Collins Saliboko, Natalie Sanford na Marin De Villard.
Alisema kuwa Tanzania itashirikisha waogeleaji 60 wakigawanywa kwa timu mbili (Tanzania A na B) chini ya makocha wao, Alex Mwaipasi na Michael Livingstone.

Nchi ambazo zimeongezewa muda wa kuthibitisha kushiriki katika mashindano ni Ethiopia, Eritrea, Somalia, Sudani Kusini ambazi zipo kanda ya tatu na za kanda ya nne ni Angola, Botswana, Comoro, Madagascar, Lesotho, Malawi, Mauritius, Seychelles, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe na Swaziland.
Alisema kuwa kwa kamati yao inatafuta wadhamini kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo. Wanahitaji kiasi cha Sh 100 milioni ili kufanya mashindano hayo kwa hadhi inayostahili.

Alisema kuwa wanatarajia waogeleaji zaidi ya 200 kushiriki katika mashindano hayo ambayo Tanzania ni mabingwa watetezi.


Hivyo makala Nchi sita kushiriki mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika

yaani makala yote Nchi sita kushiriki mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Nchi sita kushiriki mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/nchi-sita-kushiriki-mashindano-ya_10.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Nchi sita kushiriki mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika"

Post a Comment