title : MASHIRIKA 16 YA UMOJA WA MATAIFA YAZINDUA PROGRAMU YA PAMOJA KIGOMA
kiungo : MASHIRIKA 16 YA UMOJA WA MATAIFA YAZINDUA PROGRAMU YA PAMOJA KIGOMA
MASHIRIKA 16 YA UMOJA WA MATAIFA YAZINDUA PROGRAMU YA PAMOJA KIGOMA
Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii,Kigoma
MASHIRIKA 16 ya umoja wa Mataifa yamezindua programu ya pamoja mkoani Kigoma, ikiwa ni mpango wa pamoja utakaohusisha sekta mbalimbali kwa lengo la kuimarisha maendeleo na usalama kwa watu wa Kigoma.
Akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi wa programu hiyo iliyofanyika katika viwanja vya soko la pamoja lililopo katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu ,Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Paranjo alisema kuwa mpango wa programu ya pamoja utatumia njia kamilifu kutatua masuala mbalimbali yanayowakabili wakimbizi,wahamiaji pamoja na jamii za wenyeji wanaoishi Mkoa humo.
Paranjo alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma wamekuwa wakiishi na wakimbizi kwa kipindi cha muda mrefu hivyo kupitia programu hiyo na wao watanufaika.Alisema ingiwa programu hiyo ilianza Julai 1 2017 lakini uzinduzi rasmi umefanyika leo pia mpango huu utadumu kwa muda wa miaka minne.
Mkuu wa mahusiano kutoka ubalozi wa Norway Trygue Bendiksy alisema kuwa mpango huo una bajeti ya dola za kimarekani milioni 55,ambapo mpaka sasa kiasi cha dola milioni 12 kati ya hizo tayari zimeshapatikana hivyo aliwaomba wadau kuendelea kujitokeza kusaidia ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa katika programu hiyo.
Alisema mashirika hayo 16 ya umoja wa mataifa katika programu hiyo watashirikiana katika nyana za nishati na mazingira endelevu,uwezeshwaji wa kiuchumi wa vijana na wanawake,vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,elimu inayolenga wasichana wenye umri wa kuvunja ungo,maji safi pamoja na kilimo.
Mkuu wa kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Abiudi Saidaye alisema hivi sasa kambini hiyo ina jumla wakimbizi na waomba hifadhi 143608 kutoka nchi ya Burundi na Congo.Alisema mpango wa programu wa pamoja ya Kigoma utasaidia kutatua masuala mbalimbali yanayowakabili wakimbizi ikiwa ni sambamba na kuwaendeleza kimaendeleo.
Rais wa wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu Abilola Angelique kwa niaba ya wakimbizi na waomba hifadhi wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na umoja wa Mataifa kwa kitendo cha kuwapokea na kuwahudimia kwa kipindi chote walichokuwa nchini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Paranjo wakifurahi na baadhi ya wawakilishi wa mashirika ya umoja wa Mataifa baada ya kuzindua programu ya pamoja ya Kigoma
Wawakilishi wa shirika la FAO wakishirikiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma wakikabidhi zana za kilimo wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu kwaajili ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya Kigoma
Wawakilishi wa shirika la kimataifa la UNESCO wakikabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa utekelezaji wa programu ya pamoja Kigoma.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa programu ya pamoja Kigoma Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Paranjo akisoma risala yake kwenye viwanja vya soko la umoja katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu.
Rais wa kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu Abilola Angelique akiongea neno la shukrani baada ya uzinduzi wa programu ya pamoja ya Kigoma
Kikundi cha ngoma ya asili kutoka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wakitumbuiza ngoma ya asili ya kabila la warundi wakati wa uzinduzi wa programu ya pamoja ya Kigoma
Hivyo makala MASHIRIKA 16 YA UMOJA WA MATAIFA YAZINDUA PROGRAMU YA PAMOJA KIGOMA
yaani makala yote MASHIRIKA 16 YA UMOJA WA MATAIFA YAZINDUA PROGRAMU YA PAMOJA KIGOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MASHIRIKA 16 YA UMOJA WA MATAIFA YAZINDUA PROGRAMU YA PAMOJA KIGOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/mashirika-16-ya-umoja-wa-mataifa.html
0 Response to "MASHIRIKA 16 YA UMOJA WA MATAIFA YAZINDUA PROGRAMU YA PAMOJA KIGOMA"
Post a Comment