title : ANSAF YATOA DIRA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KILIMO
kiungo : ANSAF YATOA DIRA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KILIMO
ANSAF YATOA DIRA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KILIMO
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wadau wa kilimo na wakulima wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo la Kutambua na kuelewa vigezo vinavyochangia katika upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima wadogo na kutathimini mfumo wa kikanuni/ kisheria wa udhibiti wa pembejeo.
Akizungumza wakati wa mkutano huo mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano alisema kuwa waliamua kufanya utafiti kwa lengo la kumkomboa mkuliwa mdogo kuondokana na changamoto zinazomrudisha nyuma kimaendeleo.
“tunatekeleza mradi wa miaka miwili unaolenga uimarishaji utekelezaji wa sera wezeshi za kilimo na uratibu unawezesha upatikanaji wa pembejeo (mbegu, mbolea na viuatilifu) kudhibiti soko na kuhamasisha upatikanaji wake kwa wakulima wadogo” alisema Lugano.
Lugano alisema kuwa utafiti ulilenga kutazama mahitaji ya pembejeo na kiwango cha usambazaji kwa kutazama aina chache za mazao, Ufanisi wa mfumo wa kudhibiti ubora wa pembejeo za kilimo na jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau wengine katika kudhibiti biashara ya pembejeo zisizo na ubora.
“Kumekuwa na malalamiko mengi yanayohusu uwepo wa mbegu na mbolea zisizo na ubora zinazowasababishia hasara kubwa wakulima wadogo wadogo ili kutatua changamoto hizo tumekuja na huu utafiti unaoweka mambo mengi wazi na jinsi gani ya kutatua kero hizo” alisema Lugano.
Mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano akizungumza wakati wa mkutano na Wadau wa kilimo na wakulima wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) ambao una lengo la kutatua changamoto za wakulima wadogo wadogo kufikia kuwa wakulima wa kati ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuelewa vigezo vinavyochangia katika upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima.
Baadhi ya washiriki walioshiriki mkutano wa kutambulisha utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo la Kutambua na kuelewa vigezo vinavyochangia katika upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima.
Hivyo makala ANSAF YATOA DIRA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KILIMO
yaani makala yote ANSAF YATOA DIRA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KILIMO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ANSAF YATOA DIRA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KILIMO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/ansaf-yatoa-dira-ya-kutatua-changamoto.html
0 Response to "ANSAF YATOA DIRA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KILIMO"
Post a Comment