title : Waziri Mwakyembe:NIC Rudisheni Pesa za Nyumba Mlizowauzia BAKITA.
kiungo : Waziri Mwakyembe:NIC Rudisheni Pesa za Nyumba Mlizowauzia BAKITA.
Waziri Mwakyembe:NIC Rudisheni Pesa za Nyumba Mlizowauzia BAKITA.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Mchezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akitoa maagizo kwa Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Seleman Sewangi (kulia) kulitaka Shirika la Bima La Taifa (NIC) kurejesha fedha za nyumba walizowauzia kwa matumizi ya ofisi kutokana na Shirika hilo kushindwa kuwatoa wapangaji wake katika nyumba hizo huku kukiendelea kuwa na mgogoro leo tarehe 15/08/2017 jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Seleman Sewangi akimwonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Mchezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) moja ya nyumba anayoisha mpangaji aliyegoma kuhama katika nyumba hizo ambazo zimekwishauzwa kwa baraza hilo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Seleman Sewangi akimweleza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Mchezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) namna mradi wa Kongoo wanaouandaa unavyofanya kazi na utakavyosaidia mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa kutumia kompyuta katika ofisi za baraza hilo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Mchezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe ( wa kwanza kushoto) akimzungumza na mtafsiri wa Lugha ya Kiarabu Bw.Shawwaal Marinda wa Baraza la Kiswahili la Taifa (wa kwanza kulia) alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Mchezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe ( kushoto ) akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya kitabu cha kujifunza Kiswahili alichopewa kama zawadi na Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Seleman Sewangi (kulia) leo jijini Dar es Salaam alipotembelea ofisi zao.
………………………
Na Anitha Jonas – WHUSM
15/08/2017
Dar es Salaam.
Shirika la Bima la Taifa (NIC) la agizwa kurejesha pesa za nyumba walizowauzia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa matumizi ya ofisi zilizokuwa na gharama ya kiasi cha shilingi bilioni 1.5 pamoja na riba.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipotembelea ofisi hizo za BAKITA kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya baraza hilo pamoja na kutaka kufahamu namna wanavyofanya kazi.
“Kama Shirika la Bima la Taifa limeshindwa kuwaondoa wapangaji wake wakati serikali imeshakwisha kukamilisha malipo yote basi hakuna haja ya kuendelea kusumbuana ni vyema warejeshe pesa hizo ili Baraza litafute sehemu nyingine ya kununua majengo mengine ya ofisi”, alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Pamoja na hayo naye Katibu Mtendaji wa BAKITA Dkt.Seleman Sewangi alieleza kuwa malipo ya nyumba hizo walizonunua kutoka NIC kwa ajili ya matumizi ya ofisi yalishakamilika tangu mwaka 2014 lakini baadhi ya wapangaji waligoma kuhama katika nyumba hizo ambao walikuwa watumishi wa shirika hilo .
Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Waziri Mwakyembe amelitaka Baraza kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii ya kutangaza na kukuza lugha ya Kiswahili kwani taasisi hiyo ndiyo yenye dhamana ya kutangaza lugha hiyo nje na ndani ya mipaka ya nchi.
“Lugha ya Kiswahili inakuwa kwa kasi kubwa kwani tayari Umoja wa Afrika umeshaazimia kuanza kutumia lugha hiyo katika mikutano yake hivyo ni vyema kuongeza jitihada za kutengeneza mifumo thabiti itakayo rahisisha usambaaji wa lugha hii”,aliongezea Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Pamoja na hayo naye Katibu Mtendaji wa BAKITA Dkt. Selemani Sewangi alimweleza Mhe.Waziri kuwa kwa sasa Baraza linafanya Mradi wa Kongoo (Kopasi) wenye lengo la kukusanya matini zenye jumla ya maneno milioni hamsini ambazo zitakuwa chanzo muhimu cha data za kamusi na utafiti wa Kiswahili pamoja na ufundishaji wa lugha hiyo kwa kutumia kompyuta.
Hivyo makala Waziri Mwakyembe:NIC Rudisheni Pesa za Nyumba Mlizowauzia BAKITA.
yaani makala yote Waziri Mwakyembe:NIC Rudisheni Pesa za Nyumba Mlizowauzia BAKITA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mwakyembe:NIC Rudisheni Pesa za Nyumba Mlizowauzia BAKITA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/waziri-mwakyembenic-rudisheni-pesa-za.html
0 Response to "Waziri Mwakyembe:NIC Rudisheni Pesa za Nyumba Mlizowauzia BAKITA."
Post a Comment