WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA

WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA
kiungo : WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA

soma pia


WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA

Na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro
WANAFUNZI watatu wa shule  za Sekondari katika Manispaa ya Morogoro wamefariki dunia na wengine 30 kujeruhiwa miongoni mwao watu wazima baada ya basi dogo aina ya Coaster kugonga treni ya abiria iliyokuwa inatokea mikoa ya kanda ya Ziwa kuelekea Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha  tukio hilo mapema leo kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:30 asubuhi  karibu na eneo la Ofisi za Mkoa za Tanesco ambapo kipo  kizuizi cha kivuko cha treni  inapokatisha barabara ya kutoka mjini kwenda Msamvu , Manispaa ya Morogoro.
Alisema dereva aliyekuwa anaendesha basi hilo lenye  namba za usajili T438 ABR  alikatiza kwenye barabara bila kuchukua  tahadhari katika kivuko cha Treni wakati ikiwa inapita kitokea mikoa ya kanda ya Ziwa kwenda Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo alisema basi hilo ndogo linalofanya  safari zake kati ya Mjini na Kihonda  iligonga  treni hiyo ya abiria.
Kamanda Matei alisema kuwa katika ajali hiyo  wanafunzi watatu, wawili wa wakiume na mmoja wa kike walipoteza maisha na kwamba walikuwa wanasoma Shule za sekondari Tushikamane  na Mji mpya.
Kufuatia ajali hiyo  alisema polisi inamshikilia dereva wa basi hilo ndogo, Charles Damian Petro (39) mkazi wa Kihonda kutokana na kusababisha ajali iliyopoteza maisha ya wanafunzi  hao  na kujeruhi wengine kadhaa  baada ya kukatiza kwenye  kizuizi cha treni bila kuwa na tahadhari.
Kamanda Matei aliwataka wamiliki na madereva wa vyombo vya usafiri kuwa makini wakati wanapokuwa wakivuka njia za reli ili kuepusha ajali ambazo mara kadhaa zimekuwa zikisababishwa na uzembe wa madereva kwa kuzigonga treni.
Naye Mganga  mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk  Frank  Jacob  alisema , kuwa walipokea  walipokea majeruhi 33  na kati yao watatu walifariki dunia wakipatiwa matibabu  ambao ni wanafunzi , mmo akiwa ni wa kike na wawili wakiume. Alisema majeruhi 30   wamelazwa katika hospitali hiyo kati yao wanaume ni 10 na wanawake ni 23 na  hali zao zinaendelea vizuri.
Kwa mujibu wa mganga mkuu mkoa huyo  kuwa baadhi ya majina ya majeruhi waliolazwa katika wodi  namba tatu ya wanawake  ni Asha Masud, Rehma Mashaka, Fatuma Aman , Zena Shabani,  Salma Said na  Asha Omari.
Wengine ni Azama Rajab , Umi Mohamed , Magdalena Mgina , Ratifa Hassani, Florah Clemence, Eveline Mtelani, Asia Omary, Sada Seif . Lucy Lyamba, Nuru Shaban , Eliopa Paulo, Rehema Azizi na Monica Julias.
 Mbali na wodi ya wanawake majehuri wengine wanaume walilazwa katika wodi namba mbili  akiwemo Yasin Khalid Mkinngiye wanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Tushikamane.
Naye Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina  Chonjo ambaye alifika eneo la tukio hilo alisema, mashuhuda anaeleza kuwa ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva huyo.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya kuwa, askari wa reli alizuia magari kwa kunyosha alama ya kibendera chekundu kusimamisha  magari  lakini dereva huyo aliamua kuyapita yaliyosimama mbele na kufika kizuizi hicho na kabla ya kuvuka  akigonga treni hiyo.
Gari hilo liliburuzwa  umbali wa  zaidi ya mita 200  kutoka eneo la tukio na kuangukia pembezoni  na kusababisha majeruhi na vifo hivyo.
Alisema treni hiyo ya abiria  haikuwa  katika  mwendo mkali kitendo ambacho kimepunguza madhara mengi licha ya kupoteza wanafunzi watatu.
Umati mkubwa ulijitokeza eneo la ajali ambao pia walienda  kuwangalia majeruhi  wa ajali hiyo katika Hospitali hiyo ili kuwatanmbua watoto ama ndugu zao wakiwemo walimu wa shule za Sekondari na Msingi.
Basi dogo Daladala lenye  namba za usajili T 438 ABR lililokuwa  limeigonga  treni ya abiria likipelekwa kituo cha polisi
Mamia ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakwa eneo  la karibu na Ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro wakiangalia basi dogo Daladala lenye  namba za usajili T 438 ABR likiwa limeganga  treni ya abiria   yenye  kichwa namba 88U08  iliyokuwa inatokea  mikoa ya kanda ya Ziwa  kwenda Dar es salaam katika eneo la kivuko chake karibu na ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro Augosti 24, mwaka huu,  daladala hiyo ilikuwa inatokea kituo cha Masika kwenda Kihonda  ndani yake ikiwa na idadi kubwa  wanafunzi wa msingi na sekondari na wananchi.
Basi dogo Daladala lenye  namba za usajili T 438 ABR lililokuwa  limeigonga  treni ya abiria   yenye  kichwa namba 88U08  iliyokuwa inatokea  mikoa ya kanda ya Ziwa  kwenda Dar es salaam katika eneo la kivuko chake karibu na ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro Augosti 24, mwaka huu, iliyokuwa inatokea kituo cha Masika kwenda Kihonda  ndani yake ikiwa na idadi kubwa  wanafunzi wa msingi , sekondari na wananchi ikiwa juu ya gari la kubeba vitu vizito la Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kupelekwa Kituo cha Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani.
Basi dogo Daladala lenye  namba za usajili T 438 ABR lililokuwa  limeigonga  treni ya abiria   yenye  kichwa namba 88U08  iliyokuwa inatokea  mikoa ya kanda ya Ziwa  kwenda Dar es salaam katika eneo la kivuko chake karibu na ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro Augosti 24, mwaka huu. 
Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii


Hivyo makala WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA

yaani makala yote WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/wanafunzi-watatu-wafariki-dunia-baada.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA"

Post a Comment