title : Uzinduzi wa Mkutano wa Sita wa Watafiti barani Afrika wafanyika jijini Dar
kiungo : Uzinduzi wa Mkutano wa Sita wa Watafiti barani Afrika wafanyika jijini Dar
Uzinduzi wa Mkutano wa Sita wa Watafiti barani Afrika wafanyika jijini Dar
Na Agness Francis,Blogu ya jamii.
Katika kuelekea Tanzania ya viwanda awamu ya tano ipo fursa ya kushirikiana na nchi mbali mbali ili kuongeza wigo katika uchumi wa viwanda nchini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde amesema hayo katika uzinduzi wa sita wa kokangamano la utafiti barani Afrika(ARCA) kwa kushirikiana na chuo cha biashara (CBE),wakala wa vipimo (WMA) na shirika La viwango Tanzania (TBS)
Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa chuo cha biashara (CBE) katika kuelezea umuhimu wa tafiti hizo na kuleta maendeleo zaidi ya kiuchumi nchini.
Naibu Waziri Mavunde amesema kuwa serikali amewekeza fedha za kutosha vyuoni ili kuweza kufanya utafiti na nchi mbalimbali duniani, ili kukuza uchumi wa viwanda na kuweza kutoa huduma bora na bidhaa bora hapa nchini.
Awali Naibu Waziri Mavunde amesema kuwa kuwepo kwa ongezeko la viwanda nchini itasaidia kuondoa changamoto za ajira kwa vijana na kuongeza pato la taifa nchini.
Nae mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Profesa Emanuel Mjema, amesema ili kuwa na mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali lazima kuwepo na vigezo vya kupima viwango bora ili kuweza kujua takwimu sahihi kuwa ni watu wangapi wamepata huduma.
Hata hivyo Mkuregenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof. Egid Mubofu amesema kuwa tunajivunia nchi yetu kwa kukidhi vigezo vya TBS na viwango bora kulingana na viwango vyote duniani.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde akifafanua jambo kwa watafiti mbalimbali barani Afrika wakati akifungua mkutano wa sita wa watafiti barani Afrika mapema hii jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde (katikati) akikata utepe kuzindua ripoti ya sita ya utafiti barani Afrika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sayansi toka taasisi ya Applied Research Conference in Africa (ARCA) Prof. Joseph Mojekwu na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde (katikati) akionesha ripoti ya sita ya utafiti barani Afrika mara baada ya kuizindua, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sayansi toka taasisi ya Applied Research Conference in Africa (ARCA) Prof. Joseph Mojekwu na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Uzinduzi wa Mkutano wa Sita wa Watafiti barani Afrika wafanyika jijini Dar
yaani makala yote Uzinduzi wa Mkutano wa Sita wa Watafiti barani Afrika wafanyika jijini Dar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Uzinduzi wa Mkutano wa Sita wa Watafiti barani Afrika wafanyika jijini Dar mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/uzinduzi-wa-mkutano-wa-sita-wa-watafiti.html
0 Response to "Uzinduzi wa Mkutano wa Sita wa Watafiti barani Afrika wafanyika jijini Dar"
Post a Comment