title : Tawi la Exim Bank Zanzibar Yaadhimisha Miaka 20 Tokea Kuazishwa Kwake
kiungo : Tawi la Exim Bank Zanzibar Yaadhimisha Miaka 20 Tokea Kuazishwa Kwake
Tawi la Exim Bank Zanzibar Yaadhimisha Miaka 20 Tokea Kuazishwa Kwake
Msaidizi Meneja Uhusiano wa Benki ya Exim Ernest Typa akiwakaribisha wageni waalikwa katika maadhimisho ya miaka 20 ya Benki hiyo yaliyofanyika katika Tawi lake liliopo mtaa wa Mlandege Mjini Zanzibar. (kulia) Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Fedha Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar Ismail Omar Bai.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 20 ya Exim Bank Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar Ismail Omar Bai akikata keki ya miaka 20 ya benki hiyo katika sherehe zilizofanyika Tawini kwao Mlandege Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wateja wa Exim Bank walioshiriki maadhimisho ya miaka 20 ya Benki hiyo wakifuatilia sherehe hizo zilizofanyika katika Tawi lao mtaa wa Mlandege Mjini Zanzibar.
Na Khadija Khamis – Maelezo 15/08/2017.
Mkurugenzi wa Fedha Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Ismail Omar Bai amewataka wafanyabiashara na wateja wa Exim Bank kuekeza amana zao katika benki hiyo.
Akizungumza katika maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 20 ya Exim Bank yaliyofanyika katika Tawi lao lililopo Mlandege Zanzibar, alisema iwapo wafanyabiashara na wateja wataendelea kuwekeza maendeleo ya Exim Bank yatafikiwa kwa haraka .
Alisema katika kipindi cha miaka 20 tokea kuanzishwa Exim Benk imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilling za kitanzania TirionI 1.5 ikiwa ni makusanyo ya amana za wateja .
Aidha aliishauri Exim Bank kuimarisha huduma kwa wateja wao ili kuwavutia wananchi wengi zaidi kuweka amana zao na kuwa moja ya benki zenye kuleta ushindani wa kibiashara Tanzania .
Nae Meneja Mkuu wa Tawi la hilo Frederick Robert Umiro ametoa shukrani kwa wafanya biashara pamoja na wateja kwa kuwaunga mkono na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara .
Alisema Exim Bank inatowa mikopo kwa wanachama wake ikiwemo mikopo ya wafanyabiashara wadogo wadogo na wakubwa ambao huweza kukopeshwa kwa riba ya asilimia 18.
Akizungumzia mikopo ambayo huwapa wateja wao ni yamikopo mikubwa ya ujenzi wa nyumba usafirishaji bidhaa kilimo utalii na mengineo kwa lengo la kuweza kujikwamua na umasikini
Alisema Exim Bank ilianza mwaka 1997 ikiwa na tawi moja la Samora mjini Dar es salaam na hivi sasa imeweza kuengeza matawi yake kufikia 33 kwa Tanzania jambo ambalo ni maendeleo makubwa kwa Benki hiyo.
Alifahamisha kuwa katika kutanua huduma zake wamefanikiwa kufungua matawi matano Uganda, matano Visiwa vya Comorro na matawi matatu nchini Djibout.
Nae mmoja wa wateja wa Exim Bank Bi Asma Makame ameipongeza Benki hiyo kwa kuwajali wateja wao na kuwataka kuiengeza huduma ili iwe kivutio kwa wananchi wengi kujiunga .
Akieleza changamoto wanazokabiiliana nazo ni ushindani wa kibiashara na mabenki mengine ambayo kila moja hutumia mbinu za kuvuvutia wateja kwa kutumia mbinu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa unafuu katika baadhi ya huduma zao .
Hivyo makala Tawi la Exim Bank Zanzibar Yaadhimisha Miaka 20 Tokea Kuazishwa Kwake
yaani makala yote Tawi la Exim Bank Zanzibar Yaadhimisha Miaka 20 Tokea Kuazishwa Kwake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tawi la Exim Bank Zanzibar Yaadhimisha Miaka 20 Tokea Kuazishwa Kwake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/tawi-la-exim-bank-zanzibar-yaadhimisha.html
0 Response to "Tawi la Exim Bank Zanzibar Yaadhimisha Miaka 20 Tokea Kuazishwa Kwake"
Post a Comment